LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAFUNZI NA WALIMU WAJISAIDIA VICHAKANI KUTOKANA NA KUKOSA VYOO MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia, Shinyanga
Walimu na wanafunzi katika shule ya msingi Mwashimbayi iliyopo Kata ya Ngaya katika Halmashauri ya Msalala Mkoani Shinyanga, wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu kutokana na kujisaidia vichakani baada ya vyoo vya shule hiyo kutitia na kuangushwa na mvua za masika zinazoendelea kunyesha  Mkoani hapa.

Jana Diwani mteule wa Kata hiyo Mchui Charles, alisema kuwa maeneo mengi ya shule hiyo ni tambarare na imejengwa mbugani hivyo kutokana na mvua za masika kuzidi maji yalijaa uwanja mzima wa shule, na vyoo vyote kutitia hali ambayo inawalazimu kuingia vichakani kujisaidia pindi inapolazimika.

“Kwa sasa shule hii haina vyoo vya kujisaidia walimu na wananafunzi vyote vimetitia na vingine vimeanguka kutokana na hali ya eneo hili siyo zuri,mvua zikinyesha maji ya mbugani na yale ya mvua hujaa katika mazingira ya shule,suala ambalo lilipelekea vyoo kutiti”alisema Diwani.

Nae Mratibu Elimu wa Kata hiyo Zacharia Mganga alikili kutokea kwa hali hiyo na kusema kuwa taarifa za tukio hilo aliziwasilisha katika Halmashauri ya Msalala,nakuongrza kuwa endapo serikali italichukulia suala hilo kimzaha wanafunzi wanaweza kukubwa na ugonjwa wa kipindupindu.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Patrick Karangwa alisema halmashauri tayari ilikwisha toa maelekezo ya kujenga vyoo mbadala kwa kamati ya shule hiyo, wakati vikiendelea kutumika kwa mda mfupi na wanafunzi ili kuendelea na masomo wakiangalia namna ya kuanza upya ujenzi wa vyoo hivyo.

“Suala la vyoo vya shule ya msingi Mwashimbayi tumeshatoa maelekezo kwa kamati ya shule husika kujenga vyoo vya muda wakati wanafunzi wanaendelea na masomo na wakati huo tunaangalia namna ya kuwasaidia ili kukamilisha zoezi hilo". Alisema Karangwa.

No comments:

Powered by Blogger.