LIVE STREAM ADS

Header Ads

ACACIA BUZWAGI KUSADIA MILIONI 324 KATIKA UPATIKANAJI WA UMEME WA KUDUMU KAHAMA.

Na: Shaban Njia
KATIKA kuhakikisha Halmashauri ya mji wa Kahama Mkoani Shinyanga inaondokana na adha ya kukatika kwa umeme mara kwa mara, Kampuni ya ACACIA kupitia Mgodi wake wa dhahabu Buzwagi imetoa shilingi Milioni 324 kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali ili kukamilisha miundo mbinu ya umeme, inakamilika ifikapo mwezi machi mwakani.

Akizungumza jana na wandishi wa Habari ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa alisema kuna mradi wa kuondoa tatizo la umeme wilayani Kahama ambalo kwa ujumla linaotokana na uchakavu wa miundombinu ya umeme ukiwamo nguzo pamoja nguzo na nyaya zilizosimikwa tangu 1982.

Kawawa alisema kuwa kabla ya mwaka 1982 Mkoa wa Shinyanga ulikuwa ukitumia umeme unaotokana na Jenereta hali ambayo kwa sasa miundombinu yake imechakaa na kushindwa kupeleka Nishati hiyo ipasavyo katika maeneo yote yanayozunguka Mkoa wa Shinyanga.

Alisema Tanesco imeanzisha njia mbilimbili zenye urefu wa kilometa 4 na ifikapo tarehe 9 Decemba 12 juzi njia hiyo itakuwa imekamilika kwa asilimia 90 ambapo kazi itakayobaki ni kuunganisha mitambo kutoka mgodini kuja nje ya mgodi huo na kuongeza kuwa kazi hiyo itatekelezwa na wataalam kutoka katika mgodi wa Buzwagi.

“Kampuni ya Acacia kupitia mgodi wake wa Dhahabu wa Buzwagi imegharimia vifaa vyenye thamani ya Dola za kimarekani 150,000 sawa na m.324 za Kitanzania kwaajili ya kununua vifaa mbalimbali kwaajili ya kukamilisha zoezi la kutoa umeme kutoka Buzwagi kwenda katika makazi ya watu”,alisema Vita Kawawa.

Aidha kazi hiyo imeshirikisha kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya hiyo pamoja na Serikali ya mkoa na mradi huo ulianza Agost mwaka huu na Shirika la umeme Tanzania Tanesco limepewa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Decemba mwaka huu uwe umekamilika kwa kiwango cha KV 27.

Hata hivyo mkuu wa Wilaya hiyo alisema kuwa kufikia Machi mwakaujao tatizo la umeme katika Mji wa Kahama pamoja na Vijiji vyake litakuwa ni ndoto ambapo aliwataka wananchi wa mji huo kuwa wavumilivu wakati tatizo hilo likitafutiwa uvumbuzi wa haraka.

Kwaupande wake Mbunge wa jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba alisema suala la umeme katika Mji wa Kahama limekamilika kwa asilimia 90 kwani ifikapo machi 2016 wananchi wataendelea na shughuli za uzalishaji kwa kiwango kikubwa kwani tatizo hilo litakuwa limekoma.

“Niwaombe wananchi wa mji huu waendelee kuwa watulivu kwa kipindi hiki tu kwani suala la umeme katika Wilaya yetu ya Kahama limekamilika kwa asilimia 90 litakuwa limekamilika na wananhi wataendelea na shughuli zao za uzalishaji mali ili waweze kuinua uchumi wa Wilaya ya Kahama na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande Afisa mahusiano kutoka Shirika la Umeme Tanzania Mkoa wa Shinyanga Sara Libogoma alisema Shirikal lake linashirikina na Kampuni ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi katika kuhakikisha kuwa mji wa Kahama unapata umeme wa uhakika hadi kufikia mwezi machi mwaka 2016.

Libogoma aliwataka Wananchi kuhakikisha kuwa wanashirikina na Shirika la Tanesco katika kuhakikisha kuwa wanatunza vyazo vya umeme pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa kwa yeyote anayeharibu miundombinu ya umeme kwani kwa kufanya hivyo ni kutoa imani kwa waekezaji kuendelea kuwa na moyo wa kujitolea kwa mambo mengine ikiwemo kufanya marekebisho panapotokea hitilafu ndogondogo.

No comments:

Powered by Blogger.