LIVE STREAM ADS

Header Ads

HILI BARAZA LA MAGUFULI RAHA SI RAHA?

20151210035203
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DkT.John Pombe Magufuli hii leo ametangaza baraza jipya la mawaziri katika serikali yake ya awamu ya tano.

Rais Magufuli amesema baadhi ya wizara hazitakuwa na manaibu waziri, lengo likiwa ni kuwa na baraza dogo na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji ambapo kutakuwa na Wizara 18 na Mawaziri 19.

Hapa chini kuna Baraza hilo na Mawaziri na Manaibu Mawaziri wake japo baadhi hazijapata Mawaziri wake.
1.Ofisi ya Rais, Tamisemi Utumishi na Utawala Bora–Mawaziri:George Simbachawene, Angela Kairuki, Naibu:Selemani Jafo

2.Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira–Waziri:January Makamba, Naibu Waziri:Luhanga Mpina

3.Ofisi ya Waziri mkuu , Sera , Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu–Waziri:Jestina Muhagama, Manaibu: Dr Abdallah Possi, Anthony Mavunde

4.Kilimo, Mifugo na Uvuvi – Waziri: Mwigulu Nchemba, Naibu:William Nasha
5.Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Waziri: Bado hajapatikana, Naibu:Injinia Edwin Ngonyani

6.Fedha na Mipango:Waziri: Bado hajapatikana, Naibu:Ashantu Kizachi
7.Nishati na Madini–Waziri: Sospeter Muhongo, Naibu: Medalled Karemaligo
8.Katiba na Sheria – Waziri: Harrison Mwakyembe

9.Mambo ya nje, Afrika Mashariki – Waziri: Augustine Mahiga, Naibu: Suzan Kolimba
10.Ulinzi na jeshi la kujenga taifa – Waziri: Hussein Mwinyi

11.Mambo ya ndani – Waziri: Charles Kitwangwa
12.Ardhi nyumba na makazi – Waziri: William Lukuvi, Naibu: Angelina Mabula
13.Maliasili na Utalii – Waziri: Bado hajapatikana, Naibu:Ramol Makani
14.Viwanda na uwekezaji – Waziri : Charles Mwijage

15.Elimu, sayansi, Teknolojia na Ufundi – Waziri: Bado hajapatikana, Naibu:Inj. Stella Manyanya
16.Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto – Waziri: Ummy Mwalimu, Naibu:Hamis Kigwangala

17.Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo – Waziri: Nape Nnauye, Naibu: Anastasia Wambura
18.Maji na umwagiliaji: Waziri: Prof. Makame Mbarawa, Naibu: Isack Kamwela

No comments:

Powered by Blogger.