LIVE STREAM ADS

Header Ads

HAMASISHENI WANAJAMII KUJIUNGA NA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII CHF.

Judith Ferdinand, Mwanza
VIONGOZI wa Halmashauri za wilaya mkoani Mwanza wameombwa kuhamasisha  na kuelimisha jamii,  kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),ambao umelenga kuwa hudumia  watu walio katika sekta isiyo rasmi na wenye kipato duni.

Hii ni kutokana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Afya  (NHIF), kulenga zaidi watu ambao wanauwezo pamoja na ajira ya kudumu, hivyo kupitia mfuko huo ndio wakaanzisha CHF, kwa ajili ya kutoa huduma kwa kundi lililo katika sekta isiyo rasmi, ili kupata taifa bora.

Hata hivyo licha ya kuanzishwa kwa CHF,  mwitikio  wa jamii ni mdogo wa kujiunga na bima hiyo , kutokana na kutokuwa na elimu  juu ya faida inayotokana na mfuko huo , ambao kimsingi unasaidia kupata matibabu ata kama mtu atakuwa ana pesa.

Wito huo ulitolewa jana na Meneja Mwandamizi  wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Mwanza Dkt.Mkwabi Fikirini, wakati akizungumza na BMG ofisini kwake.

Fikirini alisema, viongozi wa halmashauri wanatakiwa  kufanya zoezi la kuhamasisha jamii kujiunga na CHF kuwa endelevu, kutumia angalau muda kidogo kila anapopata nafasi ya kuongea  na wananchi.

Pia aliwaomba viongozi hao kuhakikisha kila hospitali , zahanati na vituo vya afya  vilivyopo katika wilaya zao, vinakuwa na dawa, ili kusaidia jamii kujiunga na kupata matibabu anayostahili.

“Nawaomba  viongozi wa halmsahauri kuhakikisha hospitali na zahanati zinapatiwa dawa, ili mtu akiwa amejiunga na mifuko ya afya aweze kupatiwa matibabu yanayofaa bila ya kumuingiza gharama nyingine ya kununua dawa amabayo itakuwa imekosekana kati kituo achopatiwa matibabu,” alisema Fikirini.

Aidha aliwaomba viongozi hao kufanya suala la jamii  kujiunga na mfuko huo kuwa ni lazima, ili mtu aweze  kupatiwa matibabu wakati wowote hata kama  hana pesa jambo litakalosaidia serikali kupunguza gharama za matibabu.

Hata hivyo aliwaomba viongozi hao, kushirikiana na mfuko huo kuelimisha na kuhamasisha jamii kutumia huduma ya matibabu kwa njia ya bima kwani ndio mtindo wa kisasa.

No comments:

Powered by Blogger.