LIVE STREAM ADS

Header Ads

KABUCHE: SERIKALI IZIUNGANISHE KAYA MASKINI KUPITIA VIKUNDI ILI KUJIKOMBOA NA UMASKINI.

Na Judith Ferdinand, Mwanza
SERIKALI  imetakiwa kuiunganisha  jamii yenye kipato cha chini kwenye vikundi, na kuwawezesha kuanzisha miradi ili kujiinua kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi, kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), kuptia mpango wake wa kunusuru kaya maskini.

Hii ni kutokana na kuwezeshwa fedha kila baada ya muda, hali inayopelekea kaya hizo kuwa tegemezi kwa kushindwa kujiendeleza kiuchumi.

Wito huo ulitolewa jana na  Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyamanoro Mashariki  Trasisius Kabuche wakati akizungumza na BMG ofisini kwake, wilayani Ilemela mkoani hapa.

“ Naiomba Serikali iunganishe kaya maskini  kwenye vikundi kwa ajili ya   msaada kwa kushirikiana na uongozi wa kata na mtaa, ili wajiendeleze na kujiinua kiuchumi badala ya kuwapa pesa kila baada ya miezi kadhaa kupitia TASAF,” alisema Kabuche.

Alisema, endapo wataanzisha miradi kwa vikundi na kuifanya wenye itawasaidia katika suala zima la kuinua na kujiendeleza kiuchumi sambamba na kuwaajiri wengine, jambo litakaloisaidia serikali kupunguza mzigo.

Hata hivyo aliiomba serikali kuangalia upya zoezi hilo, kutokana na baadhi ya kaya zinazopata msaada huo, kutokuwa na  sifa ya uhitaji kulingana na malengo ya mradi huo.

No comments:

Powered by Blogger.