LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKURUGENZI BUKOMBE MKOANI GEITA AZIASA TAASISI BINAFSI NCHINI.

Na:Shaban Njia
TAASISI zisizo za Kiserikali nchini zimeaswa kutumia fedha za Wahisani wapatiwazo kwa kutekeleza miradi iliyokusudiwa kwa uadilifu ili kuzidi kuwashawishi wahisani hao kutoa fedha zaidi kwa ajili ya miradi ya kijamii, ambayo imekuwa kichocheo cha kusukuma gurudum la maendeleo nchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe, James Ihunyo, wakati akizungumza na viongozi wa Shirika la Huheso Foundation, lililofika kujitambulisha kuweka tawi lake wilayani Bukombe kwa lengo la kufanya kazi za Kijamii.

Ihunyo alisema Taasisi na Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanamsaada mkubwa katika maendeleo ya nchi,kutokana na kupatiwa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii ambayo husukuma maendeleo ya nchi,hivyo ni vyema kutowakatisha tamaa Wahisani kwa kutekeleza miradi iliyokusudiwa kwa uadirifu.

“Wafadhili kupitia mashirika yenu,wamekuwa msaada mkubwa kwa serikali kusukuma maendeleo ya nchi,na ili fedha hizo ziwe na tija kwa Taifa letu,ni budi kuwa waadirifu,kumbukeni ninyi mnafika maeneo ambayo serikali bado kufika,mna mchango mkubwa wa maendeleo katika nchi hii mnapotekeleza miradi hiyo ya Kijamii,”Alisema Ihunyo.

Alisisitiza uadirifu katika shughuli ili kuwatia hamasa na kuwaamini wahisani wanaowafadhili fedha  kwa ajili ya kusimamia miradi ya Kijamii kwa tija ikiwemo mapambano ya UKIMWI,Malaria,Kifua Kikuu na majanga mbalimbali na si kufuata mkumbo wa baadhi ya Taasisi ambazo zimefuja fedha za Wahisani kiasi cha kuwakatisha tamaa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali  (HUHESO FOUNDATION) Juma Mwesigwa,alimuhakikishia Mkurugenzi huyo Shirika lake litafanya kazi kwa uadirifu ili kuleta mabadiriko yenye tija wilayani Bukombe,kwa kutendea haki ufadhili watakaoupata kadri ya matakwa ya Mfadhili.

Alisema Shirika lake lililoanzishwa mwaka 2009, limetekeleza kwa uadirifu mkubwa miradi mbalimbali ya Kijamii wilayani Kahama,ikiwemo kutoa elimu za mapambano ya UKIMWI, Chakula na Lishe, Ujasiriamali, Haki za binadamu, Pesa kwa Wote na kuona umhimu wa kutanua wigo wa majukumu hayo kwa kufungua tawi wilayani Bukombe.

No comments:

Powered by Blogger.