LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIVYAWATA: SERIKALI YA AWAMU YA TANO IKUMBUKE KUWAWEZESHA WALEMAVU KIUCHUMI.

Na:Shaban Njia
CHAMA cha Walemavu Tanzania Wilaya ya Kahama (SHIVYAWATA) kimemuomba Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kuhakiksha kuwa makundi yote maalumu  yanapata haki sawa na mengine ili kuondoa dhana ya ubaguzi.

Ukiongalia kwa makundi mengine, yamekuwa yakiwezeshwa mara kwa mara aidha kupitia kwa mashirika yasiyo ya Kiserikali na hivyo kuweza kupata maendendeleo kwa haraka na kumudu maisha yao ya kila siku.

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Mkoa wa Shinyanga (SHIVYAWATA) Michael Nkanjiwa ambapo alisema kuwa wanamshukuru Rais John Magufuli kwa kutoa kibali cha kufanya sherehe za siku ya Walemavu kitaifa Mkoani Mwanza.

Mkanjiwa alisema kuwa katika Kampeni zake za kutaifuta Urais Dk,Magufuli alisema  katika utawala wake hatabagua makundi maalum hasa wenye ulemavu katika uongozi wake hali ambayo imeonyesha dhahiri kuwa amedhamiria kuwasaidia.

Katika hatua nyingine Nkajiwa alisema kuwa watu wenye ulemavu wanashindwa kukopeshaka katika taasisi za fedha kwa kuwa wanaogopa kuwa watashindwa kurejesha mikopo hiyo kutokana na hali waliokuwa nayo jambo ambalo sio la kweli na kitendo hicho ni kama kuwanyanyapaa watu wa makundi hayo.

“Tunampongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kuongoza Taifa la Tanzania na sisi  kama makundi ya watu wenye Ulemavu tumeahidi kumpa ushirikiano wa hali ya juu kutokana na utengaji wake wa kazi hali ambayo itasaidia katika kuleta mabadiliko kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kutekeleza  kauli mbio ya “hapa kazi tuu”. Alisema.

Kwaupande wake mjumbe Chama cha Walemavu Tanzania Wilaya ya Kahama (SHIVYAWATA) Edward Charles alisema kuwa  ni vema kwa Serikali kuangalia makundi kama hayo kwa sasa ili na wao pia wawe na uwezo wa kumudu changamoto nyingi zinazowakumba watu wa makundi ya Wenye ulemavu.

“Ni vema sasa kwa Serikali ya awamu ya tano Chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk,John Magufuli kuliangalia kwa macho manne kundi hilo na kuangalia changamoto mbalimbali zinazolikumba ili kuweza kuwawezesha kiuchumi na kuweza kumudu maisha yao ya kila siku” alisema Mjumbe huyo.

Alisema kuwa kwa upande wa makundi ya watu wenye Ulemavu hali imekuwa ni tofauti kidogo kwa kuwa wengi wa watu hao wamekuwa wakitegemea biashara ya kubrashi viatu au kushona hali ambayo inawafanya kuwa kama moja ya makundi yalisahaulika katika jamii na mwisho wa siku wanakuam omba omba.

“Chama chetu kwa kweli kinajitahidi katika kuhakikisha kuwa maisha yetu yanaenda vizuri lakini changamato kubwa ni mitaji ya kuweza kufanya kazi za ujasiliamali na ndio maana wengi wetu tumishia katgika kufanya kazi za kushona viatu pamoja na kupiga rangi Viatu kwa watu “Shoe Shine”, Alisema Edward Charles.

“Tumekuwa tukidhalilika sasa kwa kuombaomba kila mahali tunaomba Serikali itusadie Mitaji ya kufanyia Biashara na sisi tuweze kujitoa katika Wimbi la umasikini ambalo tupo nalo hadi kufikia hivi sasa”. Aliongeza Edward.

No comments:

Powered by Blogger.