LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUVUNJWA KWA BODI YA BANDARI YA DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amevunja bodi yote ya Bandari ya Dar es salaam na kutengua uteuzi wa Mkurugenzi mkuu wa bandari hiyo Awadhi Massawe na kumsimamisha kazi katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi Shabani Mwinjaka.

Akizungumza kwa niaba ya rais mapema hii leo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema pamoja na kuwasimamisha kazi, pia rais ameagiza wawekwe chini ya ulinzi wakati uchunguzi ukiendelea.

Aidha rais Magufuli aliwataka maafisa wanane na vigogo wanne waliohusika katika upotevu wa makontena waeleze thamani ya makontena hayo na yanamilikiwa na akinani.

No comments:

Powered by Blogger.