UHABA WA MADAWATI KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI KAHAMA, JUMLA YA WANAFUNZI 15,265 WAKAA CHINI
Na:Shaban Njia
ZAIDI ya wanafunzi 15,265 katika halmashauri ya mji wa Kahama Mkoani Shinyanga wanakaa chini wakati wa masomo kutokana na shule za msingi na sekondari kuwa na uhaba wa madawati hali ambayo inapelekea wimbi la utoro kuzidi kuongezeka,huku jumla ya madawati 11,478 yanahitaji.
Na jumla ya vyoo 1307 vya kike na kiume katika shule za msingi na sekondari vinahitaji,huku vilivyopo vinahitaji ukarabati hali mabayo wanafunzi wanakwenda kujisaidia vichana ambapo inaweza kutokea kwa magonjwa ya mlipuko hasa ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa mara baada ya ufunguzi wa baraza la kwanza la madiwani,alisema kuwa shule nyingi katika halshauri ya mji wa kahama zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyoo pamoja na madawati.
Alisema kuwa katika shule za masingi mahitaji ya madawati ni 1,144 huku yaliyopo ni madawati 572 ambapo upungufu wa madawati yanayohitaji ni 572 nakuongeza kuwa wasipolitatua tatizo hilo wimbi mloa utoro mashuleni litazidi kuongezeka.
“Ndugu zangu Madiwani katika sekta ya Elimu tunachangamoto kubwa sana hasa katika vifaa kazi kama vile,madawati,vyoo kwaajiri ya wananfunzi na walimu, hivyo nawaomba ninyi madiwani tushirikiane pamoja katika kumaliza changamoto hii japo ifikapo junuari mwaka kesho ili wanafunza watakao anza masomo wafikie katika viti nasio mkukaa chini”,alisema Kawawa.
Hata hivyo kawawa alizungumzia uhaba wa vyumba za walimu ambapo pia alitaka halmashauri kuangalia kwa makini suala hili ambapo jumla ya nyumba za walimu 1030 zinahitaji huku nyumba zilizopo ni 90,upungufu ni nyumba 941.
Kwa upande wa shule za sekondari katika halmashauri ya kahama kawawa alisema kuwa jumla ya meza na viti 14,678 vinahitajika huku mahitaji ya meza 7339, vilivyopo 6138,huku upungufu vikiwa 1161,huku mahitaji ya meza 2339,zilivyopo ni viti 698 huku upungufu ukiwani ni 1241.
Nae Mkurungezi Mtendaji wa Mji wa kahama Underson Msumba aliwataka madiwani kushirikiana vema katika kutatua changamoto katika idara ya elimu ili ifikapo januari mwaka ujao pindi masomo yatakapoanza kila mwanafunzi apate nafasi ya kuka ili kuwapatia frusa yakusoma kwa bidii nakuongeza kuwa hali hiyo itapunguza utolo mashuleni.
No comments: