LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI WAOMBA RUNGU LA MAGUFULI LA BOMOABOMOA LIMWANGUKIE MFANYABIASHARA MMOJA MJINI KAHAMA.

Na:Shaban Njia,Kahama
Mfanyabiashara mmoja Mjini Kahama Mkoani Shinyanga aitwae Paulin Mathayo amelalamikiwa kwa kuvamia eneo la wajasiriamali wa viwanda vidogo vidogo SIDO.

Mfanya biashara huyo ambaye ni mkurugenzi wa shule ya  msingi na Sekondari "Kwema" anatuhumiwa kuvamia eneo la wajasiliamali hao lililopo katika Kata ya Mwendakulima mjini hapa na kujimilikisha bila kufuata sheria na taratibu za ardhi.

Akiongea na Wandishi wa Habari, mwenyekiti wa kikundi cha wajasiliamali hao Charles Omary alisema kuwa eneo hilo walipewa na iliyokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama 1999 kama sehemu yao iliyotengwa kwaajili ya kufanyia shughuli ndogondogo za uchomeleaji vyuma.

“Eneo hilo tulilipia kwa ajili ya kuanza shughuli za uzalishaji mali lakini kwakuwa kulikuwa kunamazao yasiyohamishika ilibidi tukubali ombi la wananchi hadi wavune mazao yao ndipo tulilipie tayari kwa matumizi ya shughuli hizo kwakuwa pia Halmashauri ilituhakikishia kuwa eneo hilo ni mali yetu.”

“Kwa kuona hivyo tuliamua kusubiri, lakini katika harakati za kusubili ghafla mfanyabiashara huyo aliamua kuvamia eneo hilo kwa kujenga shule ya sekondari licha ya ku pewa barua ya kusitisha ujenzi wa sekondari hiyo na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya” alisema mwenyekiti huyo Omary.

Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba alipotakiwa kuzungumzia juu ya mgogoro huo alisema kuwa mfanyabiashara huyo yupo kihalali na amepewa hatimiliki sipokuwa eneo hilo wakwanza kupewa ni kikundi hicho cha wajasila mali hivyo weledi unatakiwa kutumika kwa mmoja kuliachia eneo hilo kwa mwenzake.

Hata hivyo mfanyabiashara huyo kila alikitafutwa na vyombo mbalimbali vya Habari amekuwa hatoi ushirikiano kwa wanahabari ikiwemo kuwaamuru walinzi kutoruhusu waandishi kuingia ofisini kwake.

No comments:

Powered by Blogger.