LIVE STREAM ADS

Header Ads

KESI YA LEMBELI YAKUPINGA MATOKE YAANZA KUSIKILIZWA.

Na:Shaban Njia
KESI ya kupinga matokeo katika Jimbo la Kahama Mjini Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imeanza kusikilizwa katika mahakama kuu kanda ya Shinyanga ambapo kesi iliyoanza kusikilizwa ni kupinga vifungu vya sheria vilivyotumika kwenye kesi ya utoaji Rushwa kwenye uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2015.

Wakili wa serikali Pendo Makondo katika kesi hiyo ambae aliwasilisha pingamizi pamoja na mwanasheria wa Mbunge wa jimbo la kahama mjini Jumanne Kishimba,Kostantine Mtalemwa alisema kuwa kifungu namba 8 chenye vifungu vya A,B,C na D vinavyohusika na Rushwa vlivyotumika katika uchaguzi huo viondolewe.

Licha ya dai hilo la kupinga vifungu kuwasilishwa na mwanasheria anayemwakilisha Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini Kostantine  Mtalemwa alisema kuwa dai hilo ni la msingi na kwamba wanaimani na mahakama itatenda haki.

Nae mwanasheria wa serikali Pendo Makondo alisema kuwa aliwasilisha pingamizi hilo katika mahakama kuu kutokana kuwa vifungu vilivyotumika katika shitaka la vitendo vya Rushwa havistahili na kwamba walichokuwa wakifanya ni kuishawishi mahakama kuviondoa vifungu hinyo.

Kwaupande wake aliyekuwa mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA James Lembeli alisema kuwa kulingana na mwenendo wa kesi unavyokwenda ni mzuri na kwamba wanachosubilia ni mahakama itatoa uamuzi wa pingamizi hilo lililowekwa na upande wa mshitakiwa pamoja na upande wa serikali.

Alisema kuwa bado anaimani kuwa mahakama kuu itatenda haki lakini akasisitiza kuwa hata kama kesi hiyo ya pingamizi akishindwa bado kesi yake ya msingi itasikilizwa kwani bado haijatajwa na kuanza kusikilizwa.

Kesi hiyo iliyoko chini ya jaji wa mahakama kuu kanda ya Shinyanga Victoria Makani alisema kuwa kutokana na maelezo ya upande wa serikali uns mlalamikaji na upande wa mlalamikiwa wa kesi hiyo itatolewa hukumu januari 08 mwaka huu baada ya mahakama kuchambua na kuona kifungu kipi kiyumike.

Awali aliyekuwa mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)James Lembeli alifungua mashitaka ya kupinga ushindi wa mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi(CCM)Jumanne Kishimba akidai kuwa mgombea huyo alishinda kutokana na kutoa Rushwa kwa wapiga kura ili waweze kumchagua.

No comments:

Powered by Blogger.