LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAABARA ZATAKIWA KUTOTOA HUDUMA ZA KIGANGA KWA WAGONJWA.

Na:Shaban Njia
Wakazi wa Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga wameitaka Serikali kupitia Wizara ya Afya Jinsia na Watoto  kupiga marufuku Maabara zisozo za kiserikali zilizopo mitaani kuwaandikia Wagonjwa dawa za kutumia pindi wanapoenda kupatiwa vipimo.

Baadhi ya Wananchi wamedai kuwa kumekuwa na tabia ya Wagonjwa kwenda kupima afya zao katika maabara hizo bila ya kuonana na daktari hali ambayo inafanya watu wengi kutumia dawa huku wasijue kuwa ni ugonjwa gani unawasumbu.

Walisema kuwa katika Mji wa Kahama kumekuwa na mrundikano wa maabara nyingi ambazo hutoa huduma ambazo hazistahi kutolewa na vituo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwaandikia Wagonjwa dawa hali ambayo kisheria hairuhusiwi kumuandika mtu dawa baada ya kupimwa.

“Ni bora Wamiliki wa maabara hizo zilizopo mitaani wakaajiri madaktari kwa ajili ya kutoa huduma huduma hizo za upimaji pamoja na matibabu kwani kwa sasa watu wengi wamekuwa wakiugua na kuandikiwa dawa katika maabara hizo bila ya kupata ushauri wa daktari husika”, Alisema Dr, Peter Kamu.

Aidha Dr, Kamu alisema kuwa ni wakati umefika kwa serikali kuliona suala hilo na kulichukulia hatua za haraka kwani huduma hizo kwa sasa katika Mji wa Kahama zimejaa kwa kiwango cha juu za kutishia afya za Wananchi ambao wamekuwa wakipatwa na matatizo ya kiafaya mara kwa mara.

“Tumekuwa tukipata shida kupata vibali kutoka maabara vya kuonyesha Mgonjwa anaumwa nini hali ambayo ukirudia vipimo unakuta anaumwa ugonjwa tofauti na hivyo kuwawia shida katika kutoa huduma za matibabu mara kwa mara”, Alisema Dr, Kamu Mganga Mkuu wa Zahanati ya Igalilimi Mjini Kahama.

Kwa upande wake Dactari Bingwa wa magonjwa ya kinywa, Sura na taya kutoka katika Hospitali ya Halmashiri ya Mji wa Kahama Samwel Mwalutambi alisema kuwa suala la utoaji huduma za kidaktari katika Maabara zilizopo mitaani ni kinyume cha sheria kutoka Wizara ya Afya.

“Mtu anaruhusiwa kutoka nyumbani kwake kwenda katika maabara yeyote kupata huduma lalini maabara hizo haziruhusiwi kumwandikia Mgonjwa huyo dawa hadi afike Hospitalini kumwona daktari”,Alisema Daktari Bingwa.

Pia Dr, Mwalutambi alisema mfumo ulipo kutoka Serikalini hauruhusiwi kwa maabara yeyote kujairi daktari na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo tayari itakuwa katika mfumo wa Zahanati hali ambayo wamiliki hao hawana kibali cha kuendesha Zahanati.

“Wamiliki wa Maabara hizo wana uhuru wa kupima mtu yeyote Yule na sii kwamwandikia dawa na pia labda Serikali ipitie upya ufumo wa kuziendesha huduma za kimaabara ikiwa ni pamoja na kuweka mipaka ya ukomo wa huduma katika vituo hivyo vya upimaji wani vimekuwa vikitoa huduma kinyume na vibali vyao vya uendeshaji vinavyoonyesha.

No comments:

Powered by Blogger.