LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAIGE: ACACIA BULYANHULU KUWENI WAZI KUHUSU MAKAMPUNI YANAYOFANYA KAZI MGODINI.

Na:Shaban Njia
MBUNGE wa jimbo la Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Ezekiel Maige amewataka Wawekezaji wa Kampuni ya Acacia inayomiliki Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu kuwa wazi kwa Halmashauri ya Msalala Kuhusu Makapuni wanayofanya nayo Biashara katika Mgodi huo.

Mbunge huyo aliyasema hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo juzi na kuongeza kuwa mapaka kufikia hivi sasa Halmashauri ya Msalala haina tawimu halisi juu ya Makampuni yanayofanya kazi mbalimbali katika Mgodi huo wa Dhahabu.

Maige alisema kuwa Kwa sasa Halmashauri ya Msalala haina budi kutengeneza makubaliano baina yao na Mgodi huo ili kuwa na mikataba ya kudumu hali ambayo Wananchi wa Wilaya hiyo wanaweza kujua hali hali ya kazi za Wafanyabiashara wanaofanya kazi na Kampuni hiyo.

Pia Maige aliitaka Halmashauri ya Msalala muhakikisha kuwa inakuwa na ofisi ndani ya Mgodi huo kwa ajili ya kudhibiti mapato mapato stahiki ambayo yanatakiwa kutolewa na Makampuni yaliopo katika Mgodi huo hali ambayo itachangia katika kukuza mapato ya ndani ya Halmashauri.

Akiongea kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Patrick Karangwa, Mweka hazina wa Halmashauri hiyo Deus Ngeranizya alisema kuwa katika Mgodi wa huo wa Acacia Bulyanhulu kuna jumla ya makampuni 25 yanayofanya kazi katika Mgodi huo hali ambayo ilipingwa vikali na Madiwani wa Halmashauri hiyo.

Madiwani hao walisema kuwa wanataka kujua jumla ya Makampuni yaliopo katika Mgodi huo ambayo yanafanya kazi na kuongeza kuwa haiwezekani kwa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu kuwa na Makampuni machache kiasi hicho kupita Mgodi wa Buzwagi mbao ni mdogo wenye jumla ya Makampuni 168 yanayofanya kazi katika Mgaodi huo.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango na Fedha ya Halmashauri ya Msalala Gerald Mwanzia alisema kuwa Kamati yake iliomba mchanganuo wa fedha hizo kutoka katika uongozi wa Acacia Bulyanhulu zlizolipwa na Makampuni yanayofanya kazi mgoni hapo lakini ilishindikana kutokana na uongozi wa Mgodi huo kushindwa kutoa ushirikiano.

Alisema kuwa baada ya kutopata ushirikiano wa kutosha kutoka Mgodini hapo Kamati hiyo haikuridhika na majibu pamoja na idadi ya Makampuni inayodaiwa kuwepo katika Mgodi huo ikiwa ni pamoja nay ale yanayofanya kazi katika Bandari ya Nchi kavu ya Isaka ambapo kuna Makampuni zaidi ya 30.

Pamoja na Mambo mengine katika kikao hicho pia Madiwani hao walipata fursa ya kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na suala la Makao makuu ya Halmashuri hiyo ambapo walikubaliana kuwa yatakuwa katika kata ya Mega badala ya Kata ya Segese na Busangi zilizokuwa zikileta msuguano hapo awali na kusababisha baadhi ya mipango ya Halmashuri hiyo kusimama.

No comments:

Powered by Blogger.