LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATU WENYE ULEMAVU MKOANI MWANZA WAILILIA SERIKALI.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (Kushoto) akimkabidhi baiskeli mmoja wa walemavu Mkoani Mwanza, Mathayo Manweki Mkazi wa Wilayani Magu. Baiske hizo zimetolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya watu wenye ulemavu Mkoani Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Chama cha Watu wenye Ulemavu Mkoani Mwanza kimeiomba Serikali pamoja na Wadau wa Maendeleo, kuweka mikakati madhubuti ya kuwasaidia watu wenye ulemavu nchini ili kuondokana na adha wanazozipata ikiwemo ukosefu wa nyenzo mbalimbali kama vile baiskeli za miguu mitatu.

Katibu wa Chama hicho Mkoa wa Mwanza Vicent Ludomya, ametoa ombi hilo hii leo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, wakati wa zoezi la kukabidhi baiskeli za walemavu (Wheel Chair) kwa watu wenye ulemavu Mkoani Mwanza ambazo zilitolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Aidha Ludomya ameishukuru Serikali kwa namna inavyowasaidia ambapo amebainisha kwamba, bado watu wenye ulemavu Mkoani Mwanza wanakabiliwa na uhitaji wa nyenzo mbalimbali ikiwemo baiskeli pamoja na magongo ya kutembelea hivyo Serikali na wadau wengine ni vema ikaongeza kasi ya kusaidia upatikanaji wa nyenzo hizo.

Nao baadhi ya Watu wenye ulemavu Mkoani Mwanza wakasisitiza zaidi juu ya suala la Serikali pamoja na Wadu wengine kujitoa kwa hali na mali katika kuwahudumia, ili kuwanusuru na hali ngumu wanayoipitia kimaisha kutokana na kukosa viungo mhimu vya mwili ambavyo vingewasaidia kujikwamua kimaisha.

Maombi hao yakamlazimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, kuzitaka halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza katika bajeti zake za Mwaka wa fedha 2016/17 kuhakikisha zinatoa majibu ya mahitaji yote ya makundi maalumu yakiwemo ya Wazee na Walemavu, vinginevyo Serikali haitazipitisha bajeti ambazo hazitakuwa na utatuzi wa mahitaji ya makundi hayo.

Mulongo hakuishia hapo, pia akazigeukia baadhi ya taasisi zinazoshindwa kutimiza wajibu wake huku zikitumia vibali vya kuwasaidia watu wenye ulemavu ambapo amezitaka halmashauri zote Mkoani Mwanza kufuatilia utendaji kazi wa taasisi hizo na kuandaa taarifa zake.

Kwa mjibu wa Jallia Mtani ambae ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Mwanza, Desemba tatu mwaka jana katika Maadhimisho ya Siku ya Walemavu Duniani yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilitoa baiskeli 11 (Wheel Chair) kwa walemavu ambapo moja kati ya baikeli hizo ilitolewa na taasisi ya Desk and Chair Foundation, ambapo baiskeli tatu zilikabidhiwa kwa walengwa katika maadhimisho hayo huku baikeli nyingine nane zilizosalia zikikabidhiwa hii leo kwa walengwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (Kushoto) akimkabidhi baiskeli mmoja wa walemavu Mkoani Mwanza, Mathayo Manweki Mkazi wa Wilayani Magu. Baiske hizo (Wheel Chairs) zimetolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya watu wenye ulemavu Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (Kushoto) akipeana mkono wa kheri na Samweli Mpina ambae ni mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ulemavu Wilayani Mavu baada ya kupokea baiskeli. Baiske hiyo ni miongoni mwa baiskeli (Wheel Chair) zilizotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya watu wenye ulemavu Mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo (Kushoto) akipeana mkono wa kheri na Christina Wilson ambae ni mama wa mtoto mwenye ulemavu kutoka Wilayani Misungwi baada ya mama huyo kupokea baiskeli kwa ajili ya mwanae. Baiske hiyo ni miongoni mwa baiskeli (Wheel Chair) zilizotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya watu wenye ulemavu Mkoani Mwanza.
Kijana Issa Ramadhani Mrisho akimsukuma mwanae Ramadhani Issa Mrisho baada ya kupokea baiskeli (Wheel Chair).

No comments:

Powered by Blogger.