MKUU WA WILAYA YA KAHAMA MKOANI SHINYANGA ATOA TAHADHARI.
Na:Shaban Njia
SERIKALI Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imewataka wazazi na Walezi wa Wanafunzi waliofaulu katika shule za Msingi na kupangiwa kwenda kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka huu katika shule za serikali kuhakikisha kuwa watoto hao wanaingia madarasani kwa muda uliopangwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa ameyasema hayo wakati akizungumza kuhusu Kamati yake ya ulinzi na Usalama ilivyojipanga katika kuhakikisha kuwa hakuna matukio ya uvunjifu wa mani katika sherehe za sikukuu ya mwaka mpya.
Kawawa aliwataka wazazi kuhakikiksha kuwa watoto waliofauli kuingia kidato cha kwanza kwa mwaka huu ikiwa ni asambamba na wale wanatakiwa kuingia katika kupata Elimu ya awali wanaingia mashuleni kwa wakatu ulipangwa hali ambayo itasadia katika kuanza masomo yao kwa muda muafaka.
“Nimewaomba Wazazi na Walezi kuhakikisha kuwa wanafunzi hao walifaulu kuingia kidato cha kwanza wanaenda shule kwa wakati pamoja na Wale waliofikia umri wa kuanza Elimu ya awali wanaanza shule mara moja katika shule walizopangiwa”, Alisema Vita Kawawa Mkuu wa Wilaya ya Kahama.
Aidha alisema kuwa katika miaka ya nyuma kumekuwa na tabia ya wazazi kuwachelewesha watoto kuingia sekondari huku wakisingizia kuwa wana matatizo ya kutafuta ada za shule pamoja na sare na kungeza kuwa hali hiyo kwa sasa haitavumiwa kabisa na ofisi yake kwani kwa kufanya hivyo ni kuwanyima watoto muda muafaka wa kupata Elimu.
Akizungumzia kuhusu hali ya usalama katika sikukuu ya Mwaka mpya , Kawawa alisema kuwa Kamati yake ya Ulinzi na usalama imejipanga vyema katika kuhakikisha kuwa hakuna matukio ya uvunjifu wa amani ambayo yangeweza kutokea katika siku hiyo na ilinzi umeiomarishwa kwa sasa.
“Sisi Kama Kamati ya Ulinzi na usalama katika Wilayah ii tumejipanga vyema na hakuna matukio yeyote yatakayoripotiwa katika sikukuu ya mwaka mpya na tunawaomba wananchi waweze kusherekea vyema bila ya kuwa na vitendo vya kuchoma matairi ovyo pamoja na matukio ya uhalifu”, Aliongeza Mkuu huyo wa Wilaya.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama aliwatakiwa wananchi wa Wilaya hiyo kusherekea siku hiyo kwa amani na upendo ikiwa ni sambamba na wale watakaokwenda kusali katika mikesha ya usiku kuhakikisha kuwa wanaimaliza kwa amani na bila ya kuwa na matukio ya fujo katika numba hizo za ibada.
No comments: