NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA).
Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni (kushoto), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa(NIDA),Dickson Maimu (kulia), wakati wa ziara ya kutembelea moja ya
ofisi za mamlaka hiyo,iliyopo barabara ya Ali Hassani Mwinyi,jijini Dar es
Salaam. Naibu Waziri aliweza kupata fursa ya kuangalia jinsi utengenezaji wa
kitambulisho cha Utaifa unavyofanyika.
Naibu Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni, akiwa katika kikao na
viongozi mbalimbali wa Vitengo vya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),wakati
wa ziara iliyoanzia Makao Makuu ya Mamlaka hiyo,jijini Dar es Salaam.Wa kwanza
kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dickson Maimu.
Afisa Msajili
wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), Emmanuel Joshua(kushoto), akitoa
maelezo jinsi taarifa za muombaji wa kitambulisho cha Taifa zinavyohakikiwa kwa
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Hamad Masauni(katikati),wakati
wa ziara ya Naibu Waziri kwenye mamlaka hiyo,jijini Dar es Salaam.
(Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
No comments: