LIVE STREAM ADS

Header Ads

TISA KITANZINI KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA KUTOKANA NA UBADHIRIFU WA FEDHA.

Na:Shaban Njia
Halmashauri ya mji wa Kahama Mkoani Shinyanga kupitia Baraza lake la Madiwani  jana limewajadili watumishi wake tisa kwa tuhuma mbalimbali za ubadhirifu wa fedha za umma pamoja na kuisababishia halmashauri hiyo hasara kupitia wadhabuni na wakandarasi waliokuwa wamepewa tenda za kufanya kazi na halmashauri hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya mkuu wa Wilaya hiyo, Vita Kawawa kutoa taarifa ya tume ya uchunguzi iliyoundwa kuchunguza ubadhilifu huo wa mapato ya ndani ambayo yalipaswa kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo iliibuliwa na wananchi kama vile Zahanati na vyumba vya madarasa.

Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka watuhumiwa hao warejeshe fedha kiasi cha shilingi milioni 150 walizokopakutoka mfuko wa fedha zinazotolewa na mgodi wa Dhahabu Buzwagi kwaajili ya ushuru wa huduma kwa wananchi(SERVICE LEV) zilizotumika kununua gari la Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kinyume na utaratibu.

Ripoti hiyo imewataka aliyekuwa Mkurungenzi wa mji huo Felix Kimaryo ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi katika Halmashauri ya Longido katika Mkoa wa Manyara pamoja na aliyekuwa Mhandishi wa Halmashauri hiyo Elick Msumba waitwe kutoa ufafanuzi juu ya ubadhilifu huo kwakuwa miradi hiyo ilikuwa chini yao.

Pia Kawawa amesema kuwa uchunguzi wa kamati hiyo ulibaini kuwa Kampuni ya Pangea Mineral inayomiliki mgodi wa Dhahabu Buzwagi ilitenga ofisi kwaajili ya Halmshauri hiyo kwa lengo la kukusanya ushuru wa huduma kwa makampuni madogomadogo yapatayo 117 yaliyomo ndani ya mgodi lakini hata hivyo imebainikakuwa kati ya hayo ni makampuni 16 ndiyo yanayolipa.

Alisema kuwa kutokana na makampuni 101 kutolipa ushuru huo imeisababishia Halmashauri kupata hasara ya jumla ya shilingi milioni 407 kwa kipindi cha Julai 14 h1di Desembq 15 mwaka jana fedha ambazo zilipaswakutumika katika shughuli za maendeleo katika kukamilisha madarasa,Zahanati pamoja na maabara ambazo tayari zilikuwa zimejengwa.

Aidha mkuu huyo wa Wilaya alilitaka baraza la Madiwani kuhakikisha linawachukulia hatua maafisa waliokuwa katika bodi ya Uzabuni kwa kudiriki kutoa tenda kwa makampuni feki ya wakandarasi kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa baadhi ya Kata huku yakiwa yamefutiwa leseni katika bodi ya ukandarasi nchini (CRB) tangu 2014 kutokana na kutolipa ada.

“Kwa hali hii, watumishi hawa tafadhali Baraza hili la Madiwani make na kuwajadili na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu kwamujibu wa sheria kwani wameisababishia Halmashauri hasara kubwav pamojan na madeni mengi kutoka kwa wakandarasi hali ambayo mpaka sasa akaunti ya fedha ya ushuru wa huduma hakuna fedha hata senti,”alisema Kawawa.

Hata hivyo Kawawa amewataja watumishi wanaotarajia kuhojiwa kuwa ni pamoja na Michael Nzingula mwenyekiti wa bodi ya uzabuni,Anastazia Manumbu,Joachim Henjewele,Alex Mrosso,Felix kimaryo aliyekuwa mkurugenzi wa mji huo,Erick Msumba ambaye kwasasa yupo katika halmashauri ya Nanyumbu, Jodan Ojode aliyekuwa kaimu mipango.

No comments:

Powered by Blogger.