LIVE STREAM ADS

Header Ads

SOKO LA IGOMBE KATIKA MANISPAA YA ILEMELA MKOANI MWANZA HATARINI.

Hili ni Soko la Igombe katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. Meza zilizotengenezwa kwa ajili ya wafanyabiashara katika Soko hilo hazitumiki na wafanyabiashara wote na badala yake baadhi ya wafanyabiashara wanaweka bidhaa zao nje ya soko hilo tena nchini pahala ambapo si salama kwa afya ya mlaji.
Hii ndiyo hali halisi. Wafanyabiashara katika Soko la Igombe wakiwa wamepanga bidhaa zao chini huku kukiwa na utiririshaji wa maji machafu ambayo hutokana na baadhi kuoshea samaki katika soko hilo hali ambayo inatishia usalama wa wafanyabiashara hao pamoja na wateja wao ikizingatiwa kwamba bado kipindupindu kinaendelea kusumbua katika Manispa hiyo.
Picha na James T kupitia namabari zetu za whatsupp 0757432694.

No comments:

Powered by Blogger.