LIVE STREAM ADS

Header Ads

BODI YA USAJI WA WAHANDISI NCHINI YATOA TAHADHARI KWA MAKAMPUNI YA UHANDISI NA WAHANDISI.

Wahandisi Washauri na Wahandisi Watalaamu Kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa Wakila Viapo vya Uhandisi hii leo Jijini Mwanza. 
Wahandisi hao wamepokea leseni ya Uhandisi ambayo itatumika kwa muda wa miaka mitatu ambapo watakaokiuka viapo vyao watanyang'anywa leseni zao na kufutiwa usajili wao.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.
Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini imeonya kuwafutia leseni Wahandisi pamoja na Makampuni ya Uhandisi nchini, Wanayokiuka sheria na maadili ya kazi yao ikiwemo kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi chini ya kiwango.

Msajili wa Bodi hiyo Mhandisi Steven Mlote, ametoa kauli hiyo hii leo Jijini Mwanza, katika Mkutano wa Kuwaapisha Wahandisi Washauri pamoja na Wahandisi Watalaamu wapatao 46 kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Wakati tahadhari hiyo ikitolewa, tayari bodi hiyo imeishayafutia Makampuni 37 ya Ujenzi pamoja na Kufuta leseni za baadhi ya wahandisi wapatao 330 nchini kwa kukiuka maadili ya kazi yao bkatika Utekelezaji wa miradi ya ujenzi.

Mhandisi Mlote amewataja baadhi ya wahandisi waliofutiwa usajili wao kuwa ni pamoja na wale waliohusika katika ujenzi wa barabara za Bariadi Mjini uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni Tisa kwa urefu wa kilomita nne na hivyo kuisababishia serikali hasara na kwamba hawatakiwi kujihusisha na shughuli za uhandisi nje na ndani ya nchini.

Wahandisi Washauri pamoja na Wahandisi Wataalamu waliokula kiapo hii leo, wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na uaminifu mkubwa kwa kuzingatia sheria na maadili ya viapo vyao ambavyo ni pamoja na kutopokea rushwa na kutekeleza shughuli za ujenzi chini ya kiwango.
Msajili wa Bodi ya Usaijili wa Wahandisi nchini, Mhandisi Steven Mlote akizungumza hii leo katika Mkutano wa Kula Viapo kwa Wahandisi kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Msajili wa Bodi ya Usaijili wa Wahandisi nchini, Mhandisi Steven Mlote akizungumza hii leo katika Mkutano wa Kula Viapo kwa Wahandisi kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Kamishna wa Viapo, Yusto Boroga ambae ni Hakimu Mkazi Mkoani Mwanza, akizungumza kabla ya kuongoza zoezi la Kuapa kwa Wahandisi Watalaamu na Wahandisi Washauri kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Kamishna wa Viapo, Yusto Boroga ambae ni Hakimu Mkazi Mkoani Mwanza, akizungumza kabla ya kuongoza zoezi la Kuapa kwa Wahandisi Watalaamu na Wahandisi Washauri kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Wahandisi Washauri na Wahandisi Watalaamu Kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa Wakila Viapo vya Uhandisi hii leo Jijini Mwanza.
Wahandisi Washauri na Wahandisi Watalaamu Kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa Wakiwa katika Mkutano wa kula Viapo vya Uhandisi hii leo Jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.