LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC MBOGWE MKOANI GEITA AHIMIZA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA.

Na Joel Maduka, Mbogwe
Imebainika kuwa wanajamii bado wanauelewa mdogo kuhusu kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya CHF Wilayani Mbogwe katika Mkoa wa Geita ambapo serikali inashauliwa kuweka mikakati kabambe ili ifanikiwe malengo iliyojiwekea ya kuhakikisha kila familia inakuwa mwanachama.

Serikali imetangaza kuwa ili kuweza kukabiliana na uhaba wa dawa na vifaa tiba nchini, kila jamii ni vyema ikajiunga na mfuko huo kwa kuchangia Sh.10,000 ambazo mwanachama atapata huduma hiyo na familia yake bure ikiwa lengo la serikali ni kuondoa ama kupunguza uhaba wa Dawa na vifaa tba Hospitalini.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Mbogwe, Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mariam Lugaira aliwahimiza madiwani wanahamiza wananchi ili wachangie kila kaya Sh.10,000 kwa ajili ya kupata huduma za matibabu ya afya kutoka Bima ya Afya.

Ndabacha Simon ambae ni diwani Kata ya Ilolangulu alipongeza mpango huo kwani ameshaanza kuona matunda hivyo ili wanajamii wote wafikiwe ili wafaidike na CHF lazima Serikali iweke mpango huo kuwa wa lazima na si ombi kwani wanajamii wengu wagumu kuelewa bila sheria na ulazima hawatajiunga na mfuko huo.

Shabani Manjaviladadi yeye ni mwanachama wa bima ya afya anapongeza mfuko huo kwa kuwa umepunguza makali ya maisha hususani kukabiliana na gharama za matibabu.

No comments:

Powered by Blogger.