LIVE STREAM ADS

Header Ads

EXCULISIVE: MAMA SHUJAA WILAYANI TARIME, ALIEPAMBANA NA JAMBAZI NA KUMNYANG'ANYA SLAA AINA YA SMG AELEZA MENGI.

Mama Sophia Steven Maguye (46) aliepambana na Majambazi mara Kadhaa Wilayani Tarime.
#‎Live kutoka kijiji cha ‪#‎Buriba-Sirari mpakani mwa ‪#‎Tanzania na ‪#‎Kenya niko na‪#‎MamaShujaa jina lake anaitwa ‪#‎Sophia Steven Maguye, ana umri wa miaka 46 ameolewa na ana watoto.

Ndie Mwanamama aliyepambana na jambazi february 9,2016 usiku wa kuamkia Feb 10, 2016 na kufanikiwa kumnyang'anya bunduki ya kivita aina ya SMG. 

Katika ‪#‎Exclusive Interview na Vesterjtz @Afya Radio ya Jijini Mwanza, mama Sophia amesema hajawahi kujiunga na jeshi lolote nchini licha ya kuvamiwia na majambazi‪ #‎Mara Mbili na kufanikiwa kuyashinda ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka #2014 na mara ya pili ni usiku wa tareh 9 kuamkia 10 mwezi wa pili mwaka 2016.

Vingi utavisikia kutoka kwake ikiwemo Maisha yake na ujasiri alionao wa kumwezesha kupambana na maadui na ataeleza kaupatia wapi ujasiri huo na mtaani wanamchukuliaje.

Pia utamsikia Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Polisi ya Tarime-Rorya, ACP GEMINI MUSHY. Kumbuka Jeshi la Polisi lilimzawadia mama huyo Shilingi Laki tano pamoja na cheti maalumu cha kutambua mchango wake katika kupambana na uhalifu hii ikiwa ni kwa ajili ya motisha.
Ni ndani ya ‪#‎96.8 Afya Radio na Vesterjtz.
BONYEZA HAPA KUSIKILIZA.

Kushoto ni Vester Joseph-Vesterjtz kutoka Afya Radio akizungumza na Mama Sophia Steven Maguye (Kulia) saliepambana na Majambazi mara Kadhaa Wilayani Tarime.

No comments:

Powered by Blogger.