LIVE STREAM ADS

Header Ads

HABARI PICHA: KILA KUKICHA AFADHARI YA JANA.

Mmoja wa akina Mama wanaofanya biashara ya kuuza mihogo kwa kuitembeza maeneo mbalimbali ya katikati ya Jiji la Mwanza, akiwa anapumzika katika eneo la Nyerere Road, katika Uga wa Bank Kuu ya Tanzania.

Picha hii imepigwa majira ya saa tisa alasiri. Ni picha yenye maana kubwa ikiwa utachukua dakika kadhaa kuitafakari. Binafsi maoni yangu ni kwamba, Wafanyabiashara ndogo ndogo (Wajasiriamali) wanahitaji kupata mwongozo sahihi wa kufanya shughuli zao ili kipato chao kiendendane na juhudi zao.

"Nadhani huyu mama anapumzika baada ya kuzunguka muda mrefu katika shughuli zake. Lakini pia anaonekana kuwa kuna jambo linamtatiza". Ameeleza mpiga picha wa gazeti moja hapa nchini wakati akiizungumzia picha hii.

Mama huyu anasema "biashara imekuwa ngumu kiasi kwamba siku hizi hata vipande vya mihogo vya shilingi 200 haviuziki sana kama ilivyokuwa mwaka jana na hii ni ishara kwamba bado hali ya mzunguko wa fedha kwa Watanzania bado haijakaa sawa".

Picha inazungumza, hivyo tuambie zaidi umeielewa vipi Picha hiyo. Email binagimediagroup@gmail.com, Whatsup 0757432694.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG

No comments:

Powered by Blogger.