LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAKAZI WA KATA YA ZENZE MANISPAA YA ILEMELA WAILILIA MAHAKAMA YA USULUHISHI WA MIGOGORO.

NA EDWIN SOKO
WAKAZI  WA MTAA  WA  ZENZE, KATA  YA  KISEKE, MANISPAA YA  ILEMELA  MKOANI MWANZA,   WAMEIOMBA  MAHAKAMA  YA  USULUHISHI WA  MIGOGORO YA ARDHI  NA NYUMBA  KUMALIZA  MASHAURI  YA   MIGOGORO  YA  ARDHI   MAPEMA  ILI KUEPUKANA NA  MIGOGORO  ISIYO  YA  LAZIMA .

HAYO YALISEMWA  NA  MWENYEKITI WA MTAA   ZENZE, SHIJA  NDUNGILE  ALIPOKUWA   AKIONGEA  NA WAANDISHI WA  HABARI  JUU  MGOGORO  WA  ARDHI   ULIOPO  KWENYE   KATA  YAKE  BAINA YA  BWANA  ALOYCE   NDAHAZA  NA  SHIRIKA  LA  UBORESHAJI WA HUDUMA  ZA KIJAMII  (MIBOS)

NDUNGILE  ALISEMA KUWA,   SHAURI  LA  SHITAKA  HILO   LIMEDUMU  MUDA  MREFU  KWENYE MAHAKAMA  HIYO   BILA  KUTOLEWA  MAAMUZI  HALI  ILIYOPELEKEA   KUKIUKWA  KWA  AMRI  YA   MAHAKAMA  YA  ZUIO  LA   MAHAKAMA (STOP  ORDER)  LA  UENDELEZAJI WA  ENEO  HILO  KUKIUKWA  NA  MLALAMIKIWA  BWANA   ALOYCE  NDAHAZA ,  KWA  KUAMUA  KUFANYA  SHUGHULI   KATIKA  ENEO  HILO  KINYUME  NA MAAGIZO YA  MAHAKAMA.

NGUNGILE  ALIONGEZA  KUWA, KUFUATIA  HALI  HIYO ILIMLAZIMU  KUIANDIKIA  MAHAKAMA  BARUA  YA  UKIUKWAJI WA  AGIZO  LA  MAHAKAMA  ILI  IWEZE  KUCHUKUA   SHERIA  STAHIKI    DHIDI  YA  BWANA  NDAHAZA.

NAYE   MWENYENKITI    WA KAMATI  YA  UPIMAJI  ARDHI  MTAA  WA ZENZE    BWANA    ABDALAH  BWILE   ALISEMA KUWA,   KUMEKUWA  NA  TABIA  KWA  BAADHI  YA WANANCHI  KUTOESHIMU   AMRI  YA  MAHAKAMA   YA  KUSIMAMISHA  UENDELEZWAJI  WA MAENENO  YENYE  MGOGORO   KABLA  YA  MAHAKAMA  ZA  ARDHI KUTOA   MAAMUZI.

PIA  AMETOA  RAI  KWA MAHAKAMA  YA  USULUHISHI WA  ARDHI  NA NYUMBA  KUJENGA   DESTURI ZA  KUMALIZA  MASHITAKA YA  ARDHI  MAPEMA  IWEZEKANAVYO  ILI  KUEPUSHA  MIGOGORO  ISIYOKUWA  YA  LAZIMA.

KWA  UPANDE WAKE  BWANA  ALOYCE  NDAHAZA  AMEKILI    KUFANYA  SHUGHULI  ZA  KILIMO  NA  IBADA  KWENYE  ENEO  HILO  LA MGOGORO KWA  KUDAI  KUWA  AGIZO  LA  MAHAKAMA  HALIKUAINISHA   SHUGHULI  ZISIZOPASWA  KUFANYWA  KWENYE  ENEO  HILO

BWANA  ELIAS  SAGAMAMBE  MKAZI WA KIJIJI  CHA    ZENZE  AMETOA  RAI  KWA  PANDE  ZOTE  MBILI  KUHESHIMU   AGIZO  ZA MAHAKAMA  LA  ENEO  HILO KUTOENDELEZWA  HADI  PALE   SHAURI   LITAKAPOTOLEWA  MAAMUZI  NA  MAHAKAMA.

No comments:

Powered by Blogger.