LIVE STREAM ADS

Header Ads

MABULA ASISITIZA SERIKALI KUTIMIZA AHADI YAKE KWA MKOA WA MWANZA.

Na Peter Fabian, MWANZA.
SERIKALI ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuri, imetakiwa kuuboresha Mkoa wa Mwanza hususani Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela kwa kuwa unachangia asilimia 13.3 ya pato la taifa ili kuendelea kuufanya Mkoa huu kuwa kuwa kitovu cha nchi za Afrika Mashariki na Maziwa Kibiashara na Kiutalii.

Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM) wakati akiwahutubia wananchi wa Kata za Igoma na Kishiri Jijini Mwanza kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya kikazi ya kusikiliza kero na kujionea changamoto mbalimbali za kijamii, kiuchumi na mazingira katika jimbo hilo.

Mabula alisema kwamba moja ya hoja atakazizipigania katika kikao cha Bunge la Bajeti ni kuhakikisha serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk Magufuli ya kuboresha Jiji la Mwanza kutokana na mchango wake huo wa pato la asilimia 13.3 kawa taifa litekelezwa ikiwemo ahadi yake aliyoitoa wakati akihitimisha kampeni za uchaguzi mkuu 2015 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mabula alisema kwamba Rais Dk Magufuli aliahidi kuboresha Mkoa wa Mwanza ikiwemo Jiji la Mwanza kuwa Gineva ya Afrika inatekelezeka kwa vitendo kutokana na Mkoa wa Mwanza kuwa wa pili kwa kuchangia asilimia 13.3 ya pato la taifa ili wananchi wake waweze kuchangamkia fursa za kiuchumi na biashara ukizingatia ukuaji wake wa asilimia 11 barani Afrika huku ikikadiliwa kuingiza wageni wa ndani na nje kwa asilimia 7.3 kila siku.

“Rais Dk Magufuli anze na kukamilishwa kwa ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mwanza, kuboreshwa kwa Reli ya Kati, kujenga barabara za lami katika wilaya za Mkoa huu ikiwemo maeneo ya katikati na pembezoni mwa Jiji la Mwanza,  Bandari ya Mwanza Kaskazini na Kusini, kuleta Meli mbili kubwa  ndani ya Ziwa Victoria,”alisema

Mbunge Mabula aliongeza kuwa  ili kuongeza mapato ya taifa na uchumi serikali haina budi kuweka mazingira kwa wawekezaji wan je na ndani kuwekeza katika sekta ya viwanda ili kuwezesha soko kwa nchi za Afrika Mashariki na Maziwa Makuu kuimalika na kuwanufaisha watanzania ukizingatia amani na utulivu iliopo.

“Tayari tunalo Jengo la Kisasa la kitega uchumi la Rock City Mall lililopo mtaa wa Ghana, Hoteli yenye hadhi ya nyota tano inayomilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) inayoendelea kujengwa eneo la Carpli point na sasa tunahitaji serikali kuboresha barabara kubwa za lami ili kuwezesha wawekezaji kuja kwa wingi mie kama mwakilishi ntapigania kwa kumkumbusha Rais Dk Magufuli,”alisema.

Mabula alisema kwamba serikali isitizame tu kuboresha Mkoa wa Dar es salaam ikiwemo Jiji hili kujengewa barabara za lami za juu, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere ikiwa ni telminal one hadi three, kujengwa ka bandari kubwa ya kisasa Mji wa Bagamoyo na koboreshwa kwa Bandari ya Dar es salaam.

Wito wangu kwa wananchi naomba tushirikiana na kumuunga mkono Rais Dk Magufuli kumkumbusha ili kuhakikisha Mwanza inapiga hatua na tuepuke watu wanaondeleza tabia ya kutugawa na kuwakataa kuwaunga mkono katika harakati zao za kutugawa kwa kutumia ukabila, dini na siasa chafu kwani uchaguzi umekwisha jukumu letu ni kupigania maendeleo ya kweli ili Mkoa na Jiji la Mwanza lifikie malengo.

No comments:

Powered by Blogger.