LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA YATUPILIA MBALI KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA KWIMBA.

Manssor akiwasalimia Wananchi wakati wa Kampeni.
Na PETER FABIAN, MWANZA
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa katika Mahakama hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana, Jimbo la Kwimba mkoani Mwanza baada ya mlalamikaji kushindwa kulipa gharama ya Sh.15 milioni aliyotakiwa kuilipa katika Mahakama hiyo.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Robert  Makaramba, alieleza mahakama hiyo kwamba uamuzi huo unatokana na mlalamikaji wake Shilogela Babila Ng’hanga aliyekuwa mgombea wa Jimbo hilo kupitia Chama Cha Demkorasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyefungua kesi Namba 5/2015 ya kupinga matokeo ya uchaghuzi jimbo hilo.

Makaramba alieleza kuwa kutokana na mlalamikaji Ng’hanga (CHADEMA) kushindwa kulipia gharama za kufungua shauri hilo pamoja na Mahakama hiyo kumpa muda wa kutosha mlalamikaji lakini ameshindwa kulipa fedha kiasi cha Sh 15 milioni kwa walalamikiwa watatu  katika kesi hiyo.

“Kimsingi uamuzi huu niliotoa ni kurejea sheria namba 111(2) ya uchaguzi mkuu, lakini mlalamikaji alipewa muda ili kulipia gharama kwa kuwalalamikia Mbunge wa sasa wa Jimbo la Kwimba, Shanif Hiran “Mansoor” (CCM), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kwimba ambaye alikuwa msimamizi msaidizi katika uchaguzi huo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali jambo ambalo hakulitekeleza.

Kwa upande wake Wakili wa kumtetea Mkurugenzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Robert Kibando alieleza Mahakamani hapo kuwa amepongeza uamuzi wa Jaji Makaramba kutokana na mlalamikaji huyo kushindwa kulipa gharama za awali ili kuwezesha kusikilizwa kesi ya msingi pia umeondoa usumbufu kwa wateja wake wa kutakiwa kufika mahakamani hapo kutoa ushahidi na kuacha kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Mansoor alisema kwamba kufatia uamuzi huo ameipongeza mahakama hiyo kwa kutupilia mbali kesi hiyo na sasa kumpa muda muafaka wa kuwatumikia wananchi waliomchagua kwa kura 39,357 (CCM) dhidi ya Ng’hanga aliyepata kura 7,338 (CHADEMA), Julius Ntiga (CUF) kura 4,079, Mchungaji Yohana Kiyuga (ADC) kura 361 na Aloyce Nzwalala (UDP), kura 0 kati ya wapiga kura halali 85,888 waliojiandikisha katika Daftari ya Tume ya Uchaguzi Jimbo hilo .

“Niombe ushirikiano wa wapiga kura wa Jimbo la Kwimba kama walivyofanya wakati walipopata taarifa za kufunguliwa kwa kesi hii ambapo pamoja na kuwashukuru kwa kunichagua walinipa moyo hivyo ni wakati wangu wa kuwatumikia kwa vitendo na kuhakikisha maendeleo yanalipaisha Jimbo la Kwimba huku pia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015/2016 ikitekelezwa zikiwemo ahadi wakati wa kampeni,”alisema.

Mansoor aliongeza kuwa mlalamikaji huyo alifungua kesi hiyo kwa madai ambayo hayakuwa na msingi kutokana na wananchi wa Jimbo hilo waliomfahamu kumkataa kwa kuwa alionekana mbabaishaji asiyeweza kuwa mwakirishi wao na atakayeweza kuzitatua changamoto za jimbo hilo, ambapo kunipa lidhaa hiyo waliona yale niliyowatum8ikia kwa miaka mitano waliponichagua mwaka 2010 ili niweze kuyakamilisha yale niliyohaidi kwao wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015.

Mlalamikaji Ng’hanga ambaye alifungua kesi hiyo bila kuweka Wakili alieleza kwa njia ya simu akiwa Wilayani Kwimba kuwa hakuweza kufika mahakamani hapo wakati wa uamuzi huo wa Jaji Makaramba baada ya ombi lake la kufungua kesi la 25Novemba 2015, kuwasilisha ombi la kupunguziwa gharama la 15 Desemba 2015  kutupiliwa mbali umemvunja nguvu na kudai kuwa sharia haiko kumsikiliza mnyonge na masikini.

“Sikuwepo Mahakamani leo (Wiki iliyopita) lakini kwa kuwa uamuzi huo umetolewa na Jaji Makaramba aliyekuwa na kesi yangu sina la kufanya zaidi ya kuziona sharia zilizopo hazitoi nafasi kwa watu wasiyo na kipato na wanyonge kwa kuwa niliomba kupunguziwa gharama lakini mahakama hiyo haikunisikiliza ikiwemo kunifanyia tathimini kama sina uwezo wa kulipa kiasi hicho,”alisema.

Mlalamikaji huyo alisema kwamba hatakata rufaa na badala yake ataendelea kujipanga na kuwaeleza wanachama wa chama chake pamoja na wananchi akipata nafasi kwenye mikutano ya hadhara ya CHADEMA kuwa uchaguzi wa Jimbo hilo matokeo yake yalichakachuliwa pamoja na kushindwa kulipia gharama ya kufungua kesi ambayo imepelekea kesi ya msingi kutosikilizwa.

No comments:

Powered by Blogger.