LIVE STREAM ADS

Header Ads

MADIWANI HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA WAPANGA MIKAKATI KUKABIRIANA NA TATIZO LA MIUNDOMBINU.

Na:Shaban Njia
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga, limemwomba Mkurugenzi wa Halmashauri  hiyo Anderson Msumba kuangalia utaratubu wa kununua mitambo ya kutengeneza barabara kwani barabara nyingi katika Halmashauri hiyo zimekuwa hazipitiki kwa muda wote.

Akiwakilisha hoja hiyo katika baraza hilo, diwani wa kata ya Kahama Mjini Hamidu Juma alisema kuwa ni bora kwa sasa Halmashauri hiyo kwa kutumia mapato yake ya ndani kuona umuhimu wa kununua mitambo hiyo kwani barabara nyingi katika Halmashauri zimekuwa hazipitiki.

Juma alisema kuwa barabara kwa sasa nyingi zimekuwa hazipitiki kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hali ambayo hata kama unakuwa na Mgonjwa anayehitajika kuwahishwa Hospitali kwa matibabu inakuwa ni vigumu kwa gari za Wagonjwa kufika katika eneo husika.

Aidha aliendelea kusema kuwa kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo ni bora hata ukanunuliwa mtambo mmoja kwanza ili barabara ziazwe kutengenezwa na kupunguza adha kwa Wananchi kuhusu suala la miundombinu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba alisema mpango huo upo lakini sio katika bajeti ya mwaka 2016/2017 bali ni katika bajeti ya 2017/2018 na tayari wamekwisha mipango imeisha kamilika na kuwa kuwataka madiwaniwani hao wasiwe na ska juu ya ununuzi wa mitambo hiyo.

Katika kikao hicho maalumu cha  Bajeti ya 2016/2017 kilifanyika mjini hapa, Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama walipitisha kiwango cha shilingi bilioni 44.1 katika kipindi hicho huku  kipaumbele cha fedha hizo kikiwa kimewekwa ni skta za miundombinu,  ajira viajana na wanawake.

Pia Halmashauri ya Mji huo imeweza kukusanya kiasi cha shilingi  Bilioni 10 kwa mwaka kama mapato yake ya ndani  ikiwa ni ongezeko la shilingi  Bilioni sita zilizokusanywa katika kipindi cha mwaka uliopita wa fedha.

Katika hatua nyingine Halmashauri hiyo katika mapatao yake ya ndani imetenga kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Haospitali ya Rufaa ya Halmashauri hiyo, Bilioni saba kwa ajili ya shughuli za maendeleo  pamoja na kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa ajili ya miundombinu.

No comments:

Powered by Blogger.