LIVE STREAM ADS

Header Ads

TASAF WATAKIWA KUZITAMBUA KAYA MASIKINI MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
Baraza la Madiwani la Halmashuri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga, limekitaka kitengo cha Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa inarudia zoezi la kuzitambua kaya masikini katika kata mbalimbali huku baadhi ya watu waliopewa msaada hawakustahili kupatiwa.

Hayo yalisemwa juzi na Diwani wa kata ya Malunga Mjini hapa Shaban Selle katika kikao maalumu kwa ajili ya kupitisha makadirio ya majeti ya Halmashuri ya Mji wa Kahama kwa kipindi cha mwaka 2016/2017.

Selle alisema kuwa Viongozi wa TASAF 111 haukuweza kuwafikia walengwa katika zoezi zima la kuwatambua hali ambayo ilifanya zoezi hilo kuwafikia watu ambao hawakuwa walengwa wa mfuko huo wa maendeleo ya jamii katika kata husika.

Aidha Sele alisema kuwa kutokana na makosa waliyoyafanya viongozi hao wa Tasaf ni bora  ufanyike upembuzi upya kwa ajili ya kuwapata walengwa halisi wa mfuko hali ambayo itapunguza manung’uniko kwa Wananchi ya kuwa mfuko ulitoa fedha kwa kaya ambazo hazikustahili.

“Zoezi hili lilifanyika kwa watu ambao hawakustahili  na pia unapowaomba viongozi wa kata wakupe orodha ya watu masikini ambao tayari wameshasaidiwa na mfuko wamekuwa wakikatalia hali ambayo imezua hofu kubwa kwa wananchi”, Alisema Shabani Selle Diwani kata ya nyihogo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Abel Shija alisema kuwa uchunguzi bora ukafanyika ili kuondoa masikitiko kwa kaya masikini ambazo hazijiwezi na pia hazijanufaika na mfuko huo wa Afya ya jamii katika kipindi hiki.

Alisema kuwa watu wamekuwa wakigawana fedha ambao hawana sifa na pia kuna wengine wakitoka kata nyingine kwenda nyingine kupata msaada huku wakisingia kuwa wao ni waathirika wa ugonjwa hatari wa Ukimwi hali ambayo mfuko huo umekuwa kwa ajili ya kunufaisha watu wachache.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama Anderson Msumba alisema kuwa ni kweli mfuko huo umekuwa na mapungufu na kuongeza kuwa zoezi la kutambua kaya masikini linasimamiwa na kamati za Vijiji na kata katika maeneoyanayohitaji msaada.

“Lazima zinufaike kaya masikini kwani zile fedha ni za serikali na zimetolewa kwa ajili ya wananchi kama hao ambao hawajiwezi na lazima wanufaike nazo kwa mujibu taraibu za Serikali zinavyoonyesha”,Alisema Anderson Msumba.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa katika zoezi lilifanyika kwa mara ya kwanza waliguindua kuwa kaya zilizoandikishwa kwa mara ya kwanza hazikuwa sahihi na kuongeza baada ya kuona hivyo ilibidi viongozi wa tasaf kurudia tena kuwatambua wananchi hao walio katika kaya masikini.

No comments:

Powered by Blogger.