LIVE STREAM ADS

Header Ads

MFANYAKAZI WA ACACIA BULYANHULU AFARIKI KWA KUGONGWA NA GARI LA MGODI.

Na:Shaban Njia
Mfanyakazi wa kampuni ya Acacia Bulyanhulu katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga Alen Chambo (32) amefariki dunia kwa kugongwa na gali lamgodi huo wakati akielekea kazini huku wengine wawili waendesha baiskeli wamenusurika kifo na kubaki na majeraha.

Kamanada wa jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga  Mika Nyange alisema tukio hilo limetokea  februari 23 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi wakati gari aina ya Land Cluiser lenye namba za usajili  T 686 ADW mali ya kampuni ya Caspian iliyokuwa ikitokea Kakola senta kuelekea mgodini hapo ndipo iliwavamia watembea kwa mguu.

“Katika ajari hiyo aliyefariki hapohapo ni Alen Chambo (32) ambaye ni mfanyakazi wa mgodini hapo na vijana wawili waendesha Baiskel waliokuwa wapita njia waligongwa na gari hilo wamejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao,mmoja ni Mayeka Mayeka (23)mkazi wa kijiji cha Usinda amevunjika mkono wa kushoto.

“Morking Masele(23)mkazi wa Igwamanoni Bugarama naye amevunjika bega la kushoto, hawa walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa matibabu zaidi”,alisema Nyange.

Hata hivyo kamanda Nyange alisema chanzo cha tukio hilo ni mwendo kasi aliokuwa nao dereva huyo na kusema Jeshi la Polisi linamshikilia dereva wa gari hilo Venans Lichard (30)mkazi wa Kakola na kwamba baada ya upelelezi atafikishwa Mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bulyanhulu John Kiganga alisema hata hivyo mfanyakazi huyo amegongwa akiwa anafanya mazoezi ya kukimbia kabla hajaingia kazini na  suala la mwendo kasi ni la kawaida kwa gari hizo hivyo ameiomba halmashauri ya Msalala kuweka matuta makubwa Kakola ili kupunguza mwendokasi wa magari.

Kiganga alisema licha ya gari hizo pia mabasi pamoja na Hiace zinazotoka mikoani huendeshwa kwa mwendo kasi ukilinganisha na barabara zote za msalala ni vumbi tupu hali ya ajali hizo ni za kawaida kutokana na vumbi kuwa jingi.

“Ili kupunguza ajali serikali ituwekee matuta ya kutosha, na hapa Kakola sehemu korofi ambako magari yanapita kwa kujisahau kuwa kuna binadamu nao wanahaki ya kutumia barabara ni Bugarama,Mwembe maua pamoja na kituo cha Mafuta Kakola watambue hapa pamesha kuwa mjini siyo machimboni tu kama wanavyofikiria,”alisema Kiganga.

No comments:

Powered by Blogger.