LIVE STREAM ADS

Header Ads

UCHELEWESHAJI WA MASHAURI UNASABABISHA MAWAKILI KUZITELEKEZA KESI NCHINI.

Na:Shaban Njia
KUKIMBIA kesi kwa baadhi ya mawakili katika Mahakama mbalimbali hapa nchini imeelezwa kuwa chanzo chake kinatokana na ucheleweshwaji wa Mashauri kukamilika katika uendeshwaji wa kesi zao Mahakamani na hivyo kufanya kesi zao kukaa muda mrefu.

Akiongea kwa niaba ya Mawakali katika Kilele cha siku ya Sheria nchini Wilayani hapa, Wakili Msomi Kelvin Munusuri Alisema kutokana na kesi wanazoenda katika Mahakama kuchelewa kumalizika mapema kumesababisha kipato chao kushuka na kupoteza muda mengi mahakamani badala ya kufanya kazi nyingine.

Wakili huyo alisema kuwa kitendo cha mashauri mengi Mahakamani kuchelewa kusikilizwa kwa wakati kunachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza Morali  wao wa kufanya kazi hali ambayo inawakatisha tamaa Wateja wao wanakwenda kutafuta huduma kwao.

Aidha alisema kuwa kama kesi moja itasikilizwa kwa muda mrefu wanapata hasara kubwa kwani kazi yao hiyo ya kutoa huduma inahitajika kwa wananchi wengi na kungeza kuwa kwa wao kushinda mahakamani kila siku wanapoteza wateja wengi wanaohitaji huduma yao.

Awali akisoma taarifa ya Mahakama hiyo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa aliyekuwa Mgeni rasmi katika sherehe hizo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama Evodia Kyaruzi alisema kuwa mahakama yake kwa mwaka jana imetihadi katika kuhakikisha kuwa mashauri waliokuwa nayo yanasikilizwa kwa wakati.

Kyaruzi alisema kuwa kwa mwaka 2015 jumla ya mashauri 1105 yalisikilizwa na kupatiwa hukumu katika 1218 yaliokuwepo  huku 113 yakibaki kitendo ambacho aliwapongeza Mahakimu pamoja watumishi wa Mahakama hiyo kwa kujitahidi katika kutoa huduma kwa Wananchi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya.

Kyaruzi pia alitoa pongezi wa Jeshi la polisi Wilaya ya Kahama, Mawakili pamoja na Watumishi wengine kwa kufanikisha kutoa huduma nzuri kwa wanachi bila ya kupokea malalamiko yanayohusu idara hiyo ya Mahakama Wilayani Kahama.

Pia Hakimu huyo aliwataka watumishi wa Mahakama kuwa wazi kwa Wananchi kuhusu kazi wanazozifanya  ili jamii iwe na imani katika uendeshwaji wa kesi zao mahakamani hapo hali ambayo itakuwa ni changamoto kubwa kwa wanachi kuelewa sheria tofauti na ilivyo kwa sasa.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kahama Vita Kawawa alisema kuwa katika Wilaya ya Kahama kuna tatizo kubwa kwa baadhi wa Wananchi kutozijua sheria kwa kuwango kikubwa hali ambayo inafanya watu wengi kuna katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya huku matatizo yao makubwa yao yakiwa ni yale ya kisheria.

Kawawa alisema pia aliwataka viongozi kutokuwa sehemu ya waamuzi ya migogoro ya kisheria  bali waelimishe Wanachi ya kupata haki katika sehemu husika hali ambayo itapunguza migogoro iliyopo ambayo sehemu inatokana na ardhi pamoja na mirathi.

No comments:

Powered by Blogger.