LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAGONJWA WA KIKE NA WAKIUME WALAZWA WODI MOJA KITUO CHA AFYA.

Na:Shaban Njia
IMEELEZWA kuwa katika kituo cha Afya kilichopo katika kata ya Ushetu Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani shinyanga wagonjwa wa kike na wale wa kiume weamekuwa wakilazwa katika wodi moja ya Wagonjwa.

Diwani wa Kata ya Ulowa katika Halmashauri hiyo Paschal Mayengo aliyabainisha hayo katika kikao cha baraza la Madiwani la Halmashauri ya Ushetu kilichofanyika  Mjini hapa na kusisitiza kuwa hali hiyo inapaswa kuangaliwa kwa haraka zaidi ili kuwanusuru wagonjwa hao.

Mayengo alisema kuwa Kituo hicho cha Afya ambacho mpaka hivi sasa kimekuwa na wodi moja tuu ya Wagonjwa kimekuwa na msongamano mkubwa wa wagonjwa hali ambayo aliishauri Halmashauri hiyo kuharakisha ujenzi wa wodi nyingine ili kuweza kuwanusuru wagonjwa.

“Haiwezekani wagonjwa wa kike na wale wa kiume kulazwa katika wodi moja hata mgonjwa akitaka kubadilisha nguo inakuwa ni kazi kwa kuwa wagonjwa wa jinsi mbili tofauti ninaomba Halmashauri ijenge wodi nyingine kwani hali hii ni hatari sana na haijawahi kutokea sehemu yeyote”, Alisema Paschal Mayengo.

Aidha Diwani huyo aliendelea kuilaumu Halmashauri hiyo kwa kuachia hali hiyo iendelee kwa muda mrefu tangu kufunguliwa kwa kituo hicho ambacho kinategemewa kuwa Hospitali ya Wilaya ya ushetu katika siku za baadaye itakapohamia katika kata ya Nyamilangano.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Halmashuri hiyo Isabela Chulumba akiongelea kuhusu sula hilo katika kikao hicho alisema kuwa Halmashauri yake kwa sasa haina fedha kwa ajili ya kuongeza wodi nyingine ya Wagonjwa katika kituo cha afya na kuongeza kuwa zoezi hilo litaweza kutekelezeka hadi katika bajeti ijayo.

“Kwa sasa Halmashauri ya ushetu haina Bajeti kwa ajili ya kuongeza wodi ya wagonjwa katika kituo cha afya cha Ushetu na kinachotakiwa ni kusubiri bajeti ijayo ya Halmashari ili kuona kama kuna uwezekano wa kuongeza wodi katika kituo hicho cha Afya”, Alisema Isabeka chilumba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu.

Hivi karibuni kumekuwa na mrundikano mkubwa wa wagonjwa katika kituo cha afya cha Ushetu kilichopo katika Halmasdhuri hiyo huku ikiwa na wodi moja tuu ya wagonjwa ambapo wagonjwa hao hulazimika kulazwa mchanganyiko bila ya kujali kuwa huyu ni mwanamke au mwanaume hali ambayo imekuwa ikipingwa vikali na baadhi wa Wananchi katika kata hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.