LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI NA WAJASIRIAMALI WAHIMIZWA KUSHIRIKI MAONYESHO YA UTALII WA KIUTAMADUNI SERENGETI.

Wakazi wa Mkoa wa Mara wakifurahia maonyesho ya Ngamia hivi karibuni.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Maonyesho  Makubwa ya Utalii wa Kiutamaduni ya Serengeti Cultural Festival, yanayofanyika kila Mwaka katika Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, yamepangwa kufanyika tena mwaka huu 2016.

Maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka, Wiki ya tatu ya Mwezi wa Saba, mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 19 hadi tarehe 21 mwezi wa Saba katika Mji wa Mugumu, Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara.

"Katika Maonyesho hayo, Watalii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi hupata fursa ya kujionea vivutio vya asili vya aina mbalimbali huku Wajasiriamali wakipata fursa ya kuonyesha na kuuza bidhaa zao za asili". Ametanabaisha Josua Nyansiry ambae ni Mwenyekiti wa kituo cha Utalii wa Kiutamaduni Serengeti (Serengeti Cultural Centre) kinachoandaa Maonyesho hayo.

Nyansiry amewahimiza Wananchi na Wajasiriamali kutoka pande mbalimbali za Tanzania na nje ya Tanzania kujitokeza ili kushiriki katika Maonyesho hayo huku akiwasihi Wajasiriamali wenye nia ya kuonyesha na kuuza bidhaa zao, kuwasiliana nae kwa simu nambari +255 (0) 784 40 21 13 ili kuthibitisha ushiriki wao.

No comments:

Powered by Blogger.