LIVE STREAM ADS

Header Ads

KESI YA WENJE NA MABULA, WAFUASI WA CHADEMA WAFURIKA VIUNGA VYA MAHAKAMA KUU.

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeanza kusikiliza Ushahidi katika Kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jimbo la Nyamagana iliyofunguliwa na aliekuwa mgombea wa Chadema Ezekiel Wenje akipinga ushindi wa Stanslaus Mabula (CCM).

Wafuasi wengi wa Chadema wamejitokeza kwa wingi kufuatilia kesi hiyo ambayo imeanza kusikilizwa asubuhi na kuahirishwa saa sita mchana kwa ajili ya kupisha muda wa chakula (lunch) ambapo itaendelea tena saa nane na nusu mchana.

Picha zote zinaonyesha wafuasi wa Chadema wakimsindikiza Wenje aliekuwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chadema Taifa akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe, kutoka viwanja vya Mahakama kwenda Gold Crest Hotel baada ya kesi hiyo kuahirishwa kwa muda ili kupisha muda wa lunch huku wakiimba nyimbo mbalimbali ikiwemo "Bila Wenje Mtatuua".
Polisi wakifanya mazungumzo na viongozi wa Chadema baada ya kutokea msongamano mkubwa wa wafuasi wa Chadema kutoka viunga vya Mahakama kwenda Gold Crest Hotel
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akitoa ufafanuzi kwa wafuasi wa Chadema kuwa kesi imeahirishwa hadi saa nane na nusu mchana.
Imeandaliwa na Binagi Blog ya Binagi Media Group.

No comments:

Powered by Blogger.