LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAKALA: KIAJANA ALIEKUFA NA BAADAE KUONEKANA AKIWA HAI MKOANI GEITA.

Na:Oscar Mihayo
Kabla hujafa hujaumbika. Ndivyo unavyoweza kusema mara baada ya kijana aliyekufa na kuzikwa kuonekana tena akiwa hai baada ya miaka miwili kupita tangu kifo chake kitokee.

Kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Nyabongo Manosa  Inaelezwa kuwa alipatwa na mauti hao akiwa kwenye biashara zake za uuzaji wa viatu huko Masumbwe  Wilaya ya Mbongwe Mkoani Geita.

Akisimulia tuki hilo  baba mzazi wa kijana huyo  Manosa Kichamo alisema kijana wake alianza kuumwa gafla na kwenda kwenye vituo mbalimbali kwa ajiri ya kupata tiba kabla ya mambo haya jawa magumu kabisa na kuamua kuuza mzigo wake na kurudi kwa wazazi.

Alisema alijitahidi kumpeleka kwa wataalam mbalimbali na ndipo alipogundulika anasumbuliwa na maralia sugu, tyfodi ya mifupa, Tb na kuanza kutumia dawa za magonjwa hayo japo nafuu haikupatikana.

Alisema licha ya kuanza kutumia dawa hizo nafuu haikupatikana kwa na ndipo alipoenda kwa wataalam zaidi a kubaini ana magonjwa ya ngono (VVU) Ukimwi licha ya kuwa bado haikurusiwa kuanza kutumia dawa za kupunguza ugonjwa huo kutokana na kuwa aliupata hivi karibuni.

Hali ya mgonjwa ilibadilika gafla na kuwa kama kichaa na ndipo alipokimbizwa kwenye Kituo cha Afya na kugundulia maralia imepanda kichwani na hivyo mnamo juni 6, 2015 saa 3:30 kijana aliiaga dunia.

Alisema taratibu za kuaga mwili zilifuatwa na mnamo juni 8 mwaka 2013 mwili wa kijana Manosa uliwasili kijijini Mwabuna kwenye makubuli ya ukoo tayari kwa kuagwa huku wananzengo, ndugu na jamaa pamoja na viongozi wa dini  wakishuhudia mazishi ya kijana huyo.

Baba mzazi aliendelea kusema kuwa mara baada ya miezi minne kupita tangu kifo cha mwanaye kitokee alichukua uamuzi wa kuhamia  majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi kama lengo la kutuliza akili yake mara baada ya kutumia kiasi kikubwa  cha pesa kama njia ya kuponesha maisha ya mwanaye .

“Nikiwa kwenye makao mapy a kwa zaidi ya miaka miwili na miezi minne  nilipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema kuwa kuna watu watatu wamaepatikana huko wilayani Masumbwe waliohofiwa kuwa walikufa na miongoni mwao walimtaja kijana wangu Nyabongo”, alisema Kichamo.

Alisema hakuamini kile alichokisia na kuamua kumpigia simu mdogo wake  Joseph Simion aishiye Shinyanga na kumtaka afike mara moja wilayani Mbongwe, na ndipo alipotekeleza agizo hilo na kufanikiwa kufika kituo cha polisi kwa ajiri ya itambuzi wa kaka yake aliyezikwa miaka miwili iliyopita.

Alisema alivyo fika polisi alijieleza na kisa kilivyokuwa  na polisi kubaki kwenye mchangao kwa kile alichokieleza mbele ya kituo hicho na ndipo alipoomba kibali kwa RPC na  afisa upelelezi kumpiga picha ili kuzisambaza kwenye mtandao wa whatsap kwa ajiri ya utambuzi zaidi kwa baadhi ya ndugu ambao wako mikoani.

Baada ya hatua hiyo kumalizika alisema alianza kuwasiliana na mdogo wake aliyeko kituoni hapo kwa kumtajia baadhi ya alama zilizoko kwenye mwili wake kama sehemu ya goti kulikuwa na kovu mara baada ya kupata ajari ya kuanguka na pikipiki na sehemu ya kinywani kuna jino lilivunjika kwenye   ajari  hiyo.
Alisema alama nyingine iliyokuwa kwenye mwili wa kijana huo alama nyeusi ya kuzaliwa maana wasukumu huiita ‘tung’ombe’ na ndipo alipomtambua kuwa kweli ni yeye kaka yake Nyabongo.

Aidha mara baada ya utambuzi huo kulionekana kitu tofautinkwenye mwili wa kijana huyo ni meno ya mbele yaliyooteshwa na kutokeza kinywani hali na nywele ndefu kama Msukule hali iliyomfanya kumuogopa kutokana na muonekano wake.

“Ndugu walifunga safari nakufika kituoni hapo kwa ajiri ya utambuzi zaidi na kuamua kuagua vilio vya kwikwi kutokana na muonekano wa ndugu yao aliyepotea kwa miaka 2 iiliyopita kabla mimi mwenyewe sijafika pale kwa ajiri kujionea hii hadithi ya peke yake” alisema Baba mzazi wa Nyabongo.

Alisema mara baada ya kutokeza mbele ya mwanangu huyo alipomwona alimkimblia kwa ajiri ya kumpokea kwa furaha na ndipo taratibu za kumutoa kituoni hapo zilifuatwa baada ya kuandika maelezo kituoni hapo na kukabidhiwa mwanangu huyo.

Mara baada ya makabidhiano hayo kufanyika alisema alitaka kujua walikompata polisi hao na ndipo walipoeleza kuwa kijana huyo alipatikana kwenye nyumba ya mfanyabiashara mmoja huko mkoani Geita mara baada ya kupigiwa simu na wasamalia wema kwenye tukio hilo lilikuwa na watu wengi sana wkitaka kujichukulia sheria mkononi.

Alisema mara baada ya kumpata mwanaye kitu cha kwanza kilikuwa ni kung’oa yale meno ambayo yalikuwa yamejitokeza kinywani kama hali ya kurudisha umbile lake la awali.

Manucho aliendelea kueleza kuwa mwanaye huyo ni kama anaanza maisha mapya mara baada ya kuanza kujifunza kila kitu kama kuvishwa nguo, kula chakula kuoga na kumpatia matibabu ya mwili ambao hajaweza kusimama na kutembea vizuri ikiwa na kuongea.

Baba mzazi huo alisema kuwa kwa sasa ameishiwa pesa kwa kuwa na hata nyumba yake aliyokuwa akiishi ameuiza kwa ajiri ya kusimamia maisha ya mwanaye hivyo kuwataka wasamalia wema na watanzania kwa ujumla kujitolea msaada wa ifedha ili kurudisha maisha ya awali ya kijana wake Nyabongo.

Nyabongo asimulia kilichotokea
Akisimulia ilivyokuwa alisema muda wote huo alikuwa amefungiwa ndani kwa mfanyabiashara Ntabo Emanueli ambaye ni binamu yake na Nyabongo.

Nyabongo aliendelea kusimulia kuwa siku anatoka ndani kwa mfanya biashara hali ilikuwa hivi, “siku hiyo familia ilitoka ikimwacha mtoto ( 9) ili muda ukifika atuletee chakula lakini alivyoleta chakula alijisahau akaleta chakula bila maji na ndipo aliporudia maji na kuuwacha mlango wazi na mimi ndipo nilipouoona mwanga huo na kuamua kutoka nje ili nione kulikoni maana miaka mingi nilikuwa sijawezaga kuuoana mwanga”

tuliletewa chakula na binti mmoja na ndipo alipofuata maji na kuacha mlango wazi namimi nikatoka kupitia mlango huo na ndipo nilipojishangaa niko kwenye watu wachafu wenye nywele ndefu”, alisema Nyabango.

Mashuhuda wazungumza
Dikson Patrick alisema ili nitukio lake la kwanza kulishuhudia kwa macho yake maana mtu waliyoamini alikufa kumbe bado yuko hai jambo linalotia aibu kwa taifa hili pindi watakaposikia tukio hili la aina yake.

Doli Charles alisema hili ni jambo la kusikitisha na kuitaka jamii kuachana na imani potofu kwani dunia ya leo mambo kama hayo yamepitwa na wakati na kuonekana na hakuna utajiri unaopitakana kwenye mambo ya kushangaza kama haya hivyo juhudi tu na kuwa na hofu ya mungu ndo vitatusaidiwa sisi kama watanzania.

Historia ya Nyabongo
Nyabongo Manosa Kichamo alizaliwa Septemba 29, 1991 huko Mwabuma wilayani Meatu Mkoani Simiyu na kusoma shule ya msingi Mwabuma kabla ya kuhamia Kishapu na kujiunga na shule ya Sekondari  Igata kabla hajafikwa na mkasa huyo akiwa kwenye biashara yake ya uuzajiwa viatu huko Masumbwe Bukombe mkoni Geita.

No comments:

Powered by Blogger.