LIVE STREAM ADS

Header Ads

MSANII ALIETEMBEA KWA MIGUU KUTOKA MWANZA HADI DAR ASEMA SHAUKU YAKE NI KUONANA NA RAIS.

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Jijini Mwanza, Joseph Stanford, maarufu kwa jina la Rich4D akiwaonyesha wanahabari Jijini Mwanza (hawapo pichani) ramani ya Mkoa wa Dar es salaam aliyoitumia kutambua maeneo ya Mkoani huo.
 Hiyo ilikuwa baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuonana na Rais John Pombe Magufuli ili kumpongeza kwa kuwajumuisha wasanii katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika baraza lake la Mawaziri. Rich4D alitembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam ili kutimiza adhma yake hiyo.

Msanii Joseph Starnford maarufu kwa jina la Rich4D alietembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam ili kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwajumuisha Wasanii katika Baraza lake la Mawaziri, amesisitiza kuwa shauku yake ni kuonana na rais ili kutimiza adhma yake.

Msanii huyo alitoa kauli hiyo jana Jijini Mwanza mbele ya Wanahabari katika hafla fupi ya kumpongeza kwa matembezi yake ya kizalendo aliyoyafanya hivi karibuni kwa ajili ya kuonana na Rais Magufuli, japo hilo halikutimia baada ya kufika Dar na kushindwa kuonana nae kutokana na rais kuwa katika majukumu mengine ya Kitaifa.

"Nilianza matembezi yangu januari 16,2016 saa kumi alfajiri na niliweza kutembea mikoa minane ambayo ni sawa na Kilomita 1,200 ambapo niliwasili Jijini Dar es salaam Februari 10,2016 ambapo nilitumia siku 26 katika matembezi hayo". Amesema Rich4D na kuongeza;

"Kila Mkoa na Wilaya nilizopita nilipokelewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Maafisa Utamaduni na baada ya kufika Dar nilipokelewa na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo aliekuwa Katibu Mkuu Omben Sefue ambae aliniahidi kuonana na Rais baada ndani ya mwezi huu". Ametanabaisha Rich4D na kumuomba Katibu Mkuu mpya Mhandisi John Kijazi kufanikisha adhma hiyo inatimia.

Lengo la Matembezi ya Rich4D ilikuwa ni kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwajumuisha wasanii katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika baraza lake la Mawaziri pamoja na kuhimiza serikali yake kutoa fursa sawa kwa wasanii wa mikoani badala fursa mbalimbali kuwagusa wasanii wa Dar pekee.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Jijini Mwanza, Joseph Stanford, maarufu kwa jina la Rich4D akiwaonyesha wanahabari Jijini Mwanza (hawapo pichani) vibali alivyokuwa navyo katika matembezi yake.

"Niwaombe wasanii wasanii wote wakubwa watoke Jijini Dar na warudi Mikoani kwao ili wakawasaidie wasanii wa Mikoani. Mfano Diamond arudi Kigoma na Fid Q arudi Mwanza na hii itasaidia kuondoa mrundikano wa wasanii Jijini Dar". Alidokeza Msanii Rich4D.
Msanii Rich4D akizungumzia matembezi yake ya Miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar. Kutoka Kushoto waliokaa ni Gaspar Babu ambae ni Meneja wa Klabu ya Fussion Jijini Mwanza ambae pia alikuwa Mratibu Msaidizi wa Matembezi ya Rich4D, Jamal Abdul ambae ni MNEC Mkoani Mwanza, Raphael Shilatu ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilayani Nyamagana, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM) Stanslaus Mabula, Alphonce Tonny Kapela ambae ni Mratibu wa Matembezi hayo.
Alphonce Tonny Kapela ambae ni Mratibu wa Matembezi hayo akizungumzia matembezi ya Msanii Rich4D ambapo amempongeza msanii huyo kwa matembezi hayo ya kizalendo.

Kutoka Kushoto waliokaa ni Gaspar Babu ambae ni Meneja wa Klabu ya Fussion Jijini Mwanza ambae pia alikuwa Mratibu Msaidizi wa Matembezi ya Msanii Rich4D, Msanii Rich4D, Jamal Abdul ambae ni MNEC Mkoani Mwanza, Raphael Shilatu ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilayani Nyamagana, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM) Stanslaus Mabula
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM) Stanslaus Mabula (kulia) amepongeza matembezi ya Msanii Rich4D ambayo ni ya kizalendo na yanayofaa kuigwa na vijana wengine. 

Mabula alijitoa kwa hali na Mali katika kusaidia Matembezi ya Msanii Rich4D baada ya kubaini mapungufu aliyokuwa nayo ikiwemo kutokuwa na pesa kwa ajili ya chakula na marazi na ameahidi kuendelea kuyasaidia makundi mbalimbali katika jamii yanayoonyesha nia na uzalendo kama wa msanii Rich4D.
Raphael Shilatu ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilayani Nyamagana (Kulia) baada ya kusikia matembezi ya Msanii Rich4D katika Vyombo vya habari ikiwemo Radio Metro Fm, alishirikiana na marafiki zake kwa ajili ya kuwezesha kukamilika kwake ikizingatiwa kwamba msanii huyo alianza matembezi hayo akiwa na akiba ya shilingi 40,000 tu.

Shilatu ambae alikuwa mgeni rasmi katika hafra hiyo amesisitiza kuwa ni vyema katibu Mkuu mpya Mhandisi John Kijazi kuhakikisha ahadi iliyoachwa na aliekuwa Katibu Mkuu Ombeni Sefue ya kufanikisha kwamba Msanii Rich4D anaonana na Rais na kuongeza kuwa yuko tayari kusimamia gharama za zote kumsafirisha kutoka Mwanza kwenda Dar es salaam. 
Picha ya Pamoja ambapo kutoka Kushoto ni Gaspar Babu ambae ni Meneja wa Klabu ya Fussion Jijini Mwanza ambae pia alikuwa Mratibu Msaidizi wa Matembezi ya Msanii Rich4D, Jamal Abdul ambae ni MNEC Mkoani Mwanza, Msanii Rich4D, Mgeni rasmi Raphael Shilatu ambae ni Mwenyekiti wa CCM Wilayani Nyamagana, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana (CCM) Stanslaus Mabula na Alphonce Tonny Kapela ambae ni Mratibu wa Matembezi hayo ya Msanii Rich4D.
Imeandaliwa na Na:George Binagi-GB Pazzo

No comments:

Powered by Blogger.