LIVE STREAM ADS

Header Ads

USIKU WA MWANAHABARI JOEL MADUKA PAMOJA NA MISS DEBORA MKAMA WAFANA JIJINI MWANZA.

Mwanahabari na Mtangazaji wa Radio Storm Fm ya Mkoani Geita ambae pia ni Mkazi wa Igoma Jijini Mwanza, Joel Maduka jana March 05,2016 amefunga pingu za Maisha na Miss Debora Jackson Roska Mkama, Mkazi wa Lumala Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Ndoa ilifungwa katika Kanisa la AICT Igoma na baadae sherehe kuhamia katika Ukumbi wa Mwanza Youth Centre uliopo Mlango Mmoja Jijini Mwanza.
Maharusi wakijiandaa kulishana keki ishara ya Upendo
Bwana Harusi Joel Maduka (Kulia) pamoja na Bibi Harusi Debora Mkama (Kulia) wakilishana keki.
Kushoto ni bibi harusi akimlisha keki mpambe (msimamizi) wake
Kulia ni bwana harusi akimlisha keki mpambe wake
Bwana harusi akiwakabidhi keki wazazi wake upande wa bibi harusi
Bibi harusi akiwakabidhi keki wazazi wake upande wa bwana harusi
It's Shampain Time,,,hahahahaaa check p!!!
Kutoka Kushoto ni mpambe wa bwana harusi, Bwana harusi, Bibi harusi na mpambe wa bibi harusi.
Maharusi wakinyweshana Shampain kwa upando kabisa
Wapambe wa maharusi nao wakapata fursa ya kunyweshana shampain ikizingatiwa kuwa hawa ni bwana na bibi
Ndugu, jamaa na marafiki wakigonga cheers na Maharusi
Ndugu, jamaa na marafiki wakigonga cheers na Maharusi
Mc Fabian kutoka Kwa Neema Radio & Famara Company Lmt akiwakilisha kwa uzuri kabisa.
Meza Kuu
Mzazi wa Maharusi upande wa Bwana harusi akitoa nasaha zake kwa Maharusi
Wazazi wa Maharusi upande wa Bibi harusi wakitoa nasaha zao kwa Maharusi.
Kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Dkt.Daniel Kulola akitoa nasaha zake kwa maharusi. Kulia ni Mama Mchungaji.
Kulia ni Mama Mchungaji wa Kanisa la  EAGT Lumala Mpya, Ilemela akitoa nasaha zake kwa maharusi. Kushoto ni Mchungaji wa Kanisa hilo Dkt.Daniel Kulola.
Wasaa wa Msosi
Ni muda wa burudani na Maharusi wakafungua Muziki kwa tabasamu mwanana
Tazama HAPA Picha za Sendoff.
Imeandaliwa na Binagi Media Group, Kupitia Binagi Blog.

No comments:

Powered by Blogger.