CHADEMA MKOANI MARA WATOA KAULI KUHUSIANA NA BUNGE KUTOONYESHWA LIVE.
Katibu waChadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche (katikati) akiwa na madiwani wa halmashauri ya Tarime Vijijini nje ya ofisi ya mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini (Chadema).
Na:Binagi Blog
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,
kimesema hakikubaliani na uamuzi wa matangazo ya shughuli za bunge kutorushwa
moja kwa moja (live), kwa kuwa hatua hiyo inawanyima wananchi kupata taarifa na
habari sahihi za bunge.
Katibu wa Chama hicho Mkoani Mara
Chacha Heche, ameyasema hayo hii leo katika ofisi ya mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini, wakati akitoa taarifa kwa wanahabari
kuhusiana na mwenendo wa uendeshaji wa shughuli za bunge ambao amesema kuwa
umekosa mwelekeo.
“Katika awamu hii ya tano, ya Serikali
inayojinasibu kuwa ni ya utumbuaji wa majipu tumeona ukiukwaji mkubwa wa katiba
ya nchi na sharia mbalimbali ikiwemo kitendo cha serikali hii kuamua kwa
makusudi kuwaficha wananchi kupata habari kutoka katika mhimili wao pekee ambao
jukumu lake ni kuwawakilisha wananchi”. Amesema Heche.
Aidha amehoji ni kwa nini serikali
inayojinasibu kuwa ni ya utumbuaji majipi, inataka majipu hayo yatumbuliwe
gizaji, huku nguvu kubwa ya dola ikitumika kuwazima wawakilishi wanaotetea
wananchi wao waone ili waone namna wanavyotenda kazi zao wawapo bungeni.
Heche ameenda mbali na kuhoji zaidi ni
kwa nini hata vyombo binafsi vya habari vimezuiliwa kurusha live matangazo ya
shughuli za bunge ikizingatiwa kwamba taarifa iliyotolewa awali na Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh.Nape Nhauye ya kutorusha matangazo hayo
live kupitia shirika la taifa la utangazaji TBC ni uhaba mdogo wa gharama za uendeshaji.
“Rais wa awamu ya utumbuaji majipu
alisema mwenyewe atawatumbua watendaji wa serikali mchana kweupe kwa kuwa
aliwateua yeye tena na kuwatangaza hadharani, sasa iweje sisi wananchi ambao
tuliwachagua wabunge wetu kwa kura mchana tuonyweshwe wanachojadili usiku, tena
kipindi kilichorekodiwa wakati sisi tuliwachagua live baada ya kuwasikiliza
live”. Amehoji Heche.
No comments: