LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAFANYAKAZI KUFANYIKA NJE YA JIJI LA MWANZA.

Judith Ferdinand,Mwanza
Maadhimisho ya siku ya  wafanyakazi duniani (mei mosi) mkoani Mwanza, yanatarajiwa kufanyika wilayani Misungwi huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa John Mongella.

Maadhimisho hayo yanayofanyika kila mwaka tarehe 1 mwezi mei, ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni "Dhana ya mabadiliko ilenge kuinua hali za wafanyakazi".
Katibu wa Shirikisho la Vyama huru vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Mkoani Mwanza, Zebedayo Athuman, jana alisema, kaulimbiu ya mwaka huu imelenga kuhimiza serikali kuwainua wafanyakazi kutoka hali duni.

Alisema watahimiza serikali  kuongeza mishahara kwa wafanyakazi ili kima cha chini kianzie sh. 750,000 na kwamba waajiri wanapaswa kuwaruhusu wafanyakazi wao kushiriki katika maadhimisho hayo.

No comments:

Powered by Blogger.