LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC KIGOMA AHOFIA KUTUMBULIWA, AWAOMBA WADAU KUOKOA JAHAZI.

Na Rhoda Ezekil, Kigoma
Kutokana na upungufu wa madawati 74,456  Mkoani Kigoma, Mkuu wa Mkoa huo Brigedia jenerali Emanuel Maganga, amewaomba wadau wa maendeleo na wamiliki wa mashirika mbalimbali wakiwemo watumishi wa umma kuchangia madawati ili kuepukana na changamoto hiyo.

Akiwaomba wadau hao katika kikao cha kuchangia madawati kilichofanyika ofisini kwake jana, Maganga alisema ni agizo la Rais ifikapo june 30 mwaka huu kusiwepo mwanafunzi atakae kaa chini kutokana na ukosefu wa madawati.

"Ili niendelee kuwa Mkuu wa Mkoa, niwaombe ndugu zangu tuendelee kushirikiana, mchangie madawati na ahadi mtakazotoa zikamilike kabla ya mei 30 mwaka huu ili tuweze kutekeleza agizo agizo la rais kwa wakati". Alisema Maganga.

Hata hivyo kwa kuona umuhimu wa jambo hilo, alianza kwa kuchangia dawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni tano, ili kuweza kukabiliana na changamoto ya madawati katika Mkoa huo na kuwahimiza Wakuu wa Wilaya na wakuu wa taasisi za umma kuchangia madawati 50 kwa kila mmoja.

Afisa elimu Mkoa wa Kigoma, Jelumana Mng’ong’o, alisema changamoto za madawati zinasababisha kero kadhaa ikiwemo uwezo wa wanafunzi kushuka kitaaluma, kupunguza usikivu kwa wanafunzi, kushindwa kuumba herufi  na kumfanya mwalimu kutumia nguvu katika kutafuta mbinu za ufundishaji.

No comments:

Powered by Blogger.