LIVE STREAM ADS

Header Ads

INASIKITISHA, AJALI KASULU MKOANI KIGOMA YASABABISHA VIFO.

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
Watu wawili wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Hiace yenye no T.502 BKY iliyogongana na gari no T.321BHC Bus Scania katika Kijiji cha Bugaga kata ya Bugaga, tarafa ya Heru Chini, kasulu Mkoani humo.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma,SACP,Fredinandi Mtui aliwataja walio fariki katika ajali hiyo ni,Essau Johnson muha miaka 20 Mkazi wa Kijiji cha Bugaga na Mwanamke mmoja ambae jina lake halikufahamika.

Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 17aprili majira ya saa kumi na moja jioni huko katika kijiji cha Bugaga Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma lilisababishwa na mwendo kasi wa dereva.

Mtui alisema kuna majeruhi wawili walio jeruhiwa katika ajali hiyo na chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa Hiace uliopelekea kushindwa kulimudu gari lake kisha kuligonga basi hilo walipo kuwa wakipishana darajani.


"Baada ya ajari hiyo kutokea dereva aliefahamika kwa jina la,Sologo Nkeshimana Mkazi wa Kijiji cha Mwandiga Wilaya ya Kigoma vijijini alikimbia baada ya kusababisha ajali hiyo",alisema Mtui.

Alisema majeruhi wote wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya kasulu na hali zao zinaendelea vizuri na dereva alie sababisha ajali hiyo anaendelea kutafutwa iliaweze kufikishwa mahakamani.

Jeshi la polisi Mkoani humo linawaomba madereva wote kutii sheria na kufuata Sheria za Usalama Barabarani ilikupunguza vifo na majeruhi vinavyo tokana na uzembe wa madereva wazembe.

No comments:

Powered by Blogger.