LIVE STREAM ADS

Header Ads

KATIBU MKUU UVCCM TAIFA AFANYA ZIARA MKOANI ARUSHA.

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka (wa tatu kushoto mbele) akitoka kusaini daftari la wageni katika Ofisi kuu ya UVCCM Mkoa wa Arusha baada ya kufanya ziara katika Mkoa huo jana. Pembeni yake ni Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa Wa Arusha Lengai Ole Sabaya.

Pamoja na shughuli nyingine katika ziara hiyo, Shaka alifanya uzinduzi wa Shina la vijana wakereketwa wa CCM la "Hapa Kazi Tu" lililopo katika Kata ya Sinuni Mkoa wa Arusha.

Pia alihutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara wa ufunguzi wa kampeni za Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Mapya katika kata ya Sinoni Mkoani Arusha.
Kwa sasa Shaka anashikilia nafasi ya Katibu Mkuu UVCCM baada ya Sixtus Mapunda aliekuwa Katibu UVCCM Taifa kuchaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini Mkoani Ruvuma.
Picha na Fahad Miraji; Arusha

No comments:

Powered by Blogger.