LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANAMUZIKI PAPAA WEMBA AFARIKI DUNIA.

Mwanamuziki wa siku nyingi Jules Shungu Wembadio Pene, maarufu kwa jina la Papaa Wemba amefariki duni usiku wa kuamkia leo akiwa Abidjan nchini Ivory Coast alikokuwa ameenda kwa ajili ya kufanya shoo. 

Binagi Blog imepata duru za habari zinazoeleza kwamba, Papaa Wemba alifariki dunia akiwa hospitalini alikokimbizwa baada ya kuanguka na kupoteza fahamu, wakati akitumbuiza jukwaani.
Amefariki akiwa na miaka 67 ikikumbukwa kwamba alizaliwa tarehe 14 mwezi June, Mwaka 1949 katika Wilaya ya Sankuru nchini Congo. 
R.I.P Papa Wemba. Mashabiki wa muziki wa hususani wapenzi wa Soukous watakukumbuka daima kwa umahiri wako katika muziki.

                           Imeandaliwa kwa Msaada wa Mtandao

No comments:

Powered by Blogger.