LIVE STREAM ADS

Header Ads

OJADACT WALAANI VIKALI WAANDISHI WA HABARI KUZUIWA KUINGIA BUNGENI KUFANYA COVERAGE.

Mwenyekiti wa Ojadact, Edwin Soko
Ndugu waandishi wa Habari, wanaharakati na watanzania wote.
Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Tunalaani vikali kuzuiwa kwa Waandishi kuingia Bungeni kwa lengo la kufanya coverage (kuandaa habari) ya vikao vya Bunge la kujadili mpango wa maendeleo ya miaka mitano na bajeti ya serikali.

OJADACT, hatukubaliani na utaratibu wa sasa wa kutumia idara ya habari na maelezo ya Bunge, kuwa ndio wenye jukumu la kukusanya taarifa na kuzigawa kwa waandishi.

Ni ukweli usiopingika kuwa, maamuzi hayo yana athari zifuatazo.
Kuminya uhuru wa haki ya kupata taarifa kwa wananchi km ilivyoainishwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano.wa.Tanzania ibara ya 18.

Kuminya uhuru wa vyombo vya habari, ambao umekuwa ukikosa haki ya msingi  iliyokosekana kwenye Katiba.

MSIMAMO WETU.
Kwa kuwa Bunge  halioni umuhimu wa waandishi Bingeni basi tunaviomba vyombo vyote vya habari vya binafsi kuwatoa waandishi wao bungeni.

Tunaviomba vyombo vyote vya habari vya binafsi kususia kuandika habari za bunge hadi hapo litakapotengua utaratibu huo.

Waziri mwenye dhamana ya habari afute kauli yake ya kejeli kuwa wanaopinga utaratibu huo eti waende Mahakamani.

Ahsanteni sana wanahabari kwa kuitikia wito wetu.
Edwin Soko
Mwenyekiti
April 24,2016
Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.