LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWILI WA MAREHEMU HENRY KIHERILE WAAGWA NCHINI MAREKANI.

Jioni ya jana Jumamosi (16/04) Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la Houston na miji mingine ya karibu ilifanya Ibada Takatifu katika kanisa la Umoja kumuaga mpendwa wao Henry Kiherile aliyefariki wiki moja na nusu iliyopita baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana. 

Ibada hiyo ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa na huzuni kubwa juu ya kifo hicho kilichogusa mioyo ya watu wengi. 

Mwili wa marehemu Henry unatarajiwa kusafirishwa jioni ya leo kuelekea nyumbani Tanzania kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa tarehe 22/04/2016. Pata picha za Misa hiyo hapa chini.
Marehemu Henry Kiherile enzi za uhai wake

No comments:

Powered by Blogger.