LIVE STREAM ADS

Header Ads

PUMZIKA KWA AMANI DJ ALEX DA WOLF, WEMA WAKO UTADUMU MILELE.

Alex Masatu maarufu kwa jina la Dj Alex Da Wolf enzi za uhai wake akiwa katika Kituo cha Radio Metro Mwanza.
Dj Alex Da Wolf alikuwa ni miongoni mwa Madjz Wakongwe nchini Tz ambao walipata kufanya kazi katika vituo mbalimbali vya redio pamoja na Klabu nchini, ikiwemo redio Metro Fm Mwanza.

Mchango wake katika kuukuza muziki wa wasanii wachanga ni mkubwa kuliko inavyodhaniwa. Zamani Dj kucheza wimbo wa msanii chipukizi akiwa klabu au redioni ilikuwa mbinde, lakini Da Wolf hakuwa na kinyongo, kwani aliweza kucheza nyimbo za wasanii hao bila ugumu wowote.

Hakika chema hakidumu, Da Wolf alifariki duni April 21,2014 katika ajali ya basi la Luhuye lililopata ajali katika eneo la Masanza Kona Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, likitokea Tarime Mkoani Mara kuja Mwanza. 

Da Wolf alikuwa mmoja wa abiria 11 waliopoteza maisha papo hapo katika ajali hiyo mbaya, huku kesho yake idadi ya vifo ikiozgezeka na kufikia 16. Abiria wengine wengi walijeruhiwa na idadi yao ilifikia 35. Chanzo cha ajali hiyo kilielezwa kuwa ni mwendo kasi.

Pumzika kwa Amani, Dj Alex Da Wolf. Ulikuwa mtu wa watu. Mchapa kazi. Hadi mauti yanakupata ulikuwa ukitoka katika shughuli zako za U-Dj wakati ukitoka kupiga muziki katika kusherehekea sikukuu ya Pasaka 2014. Hakika wema hawadumu ila upendo wako utadumu milele mioyoni mwetu.

No comments:

Powered by Blogger.