LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATU 19 WATIWA MBARONI KAHAMA MKOANI SHINYANGA.

Na:Shaban Njia
Watu 19 wanaosadikika kuwa ni wahamiaji haramu wanashikiliwa na polisi katika Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga.

Inaelezwa kwamba watu hao wanatoka katika nchi za Rwanda, Burundi na Uganda ambapo wanashirikiwa kutokana na makosa ya kuishi nchini bila kuwa na vibali.

Afisa Uhamiaji Mkoani Shinyanga, Annamaria Yondani, ameyasema hayo wakati akizungumza na wahabari ofisini mwake.

"Wahamiaji hao wamegawanyika katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza ni wale waliongia nchinikwa lengo la kufanya biashara huku kundi la pili likiwa ni wanaoikingia kufanya matembezi huku kundi la tatu llikiwa ni wale wanaongia nchini bila kufuata utaaratibu". Alisema Yondani.

Alitoa rai kwa wananchi Mkoani Shinyanga kuwafichua watu wanaoishi nchini bila kibali huku akiwataka wale wote wanaoishi Mkoani humo bila kibali kujisalimisha.

No comments:

Powered by Blogger.