LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTATURU: CCM ITASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA MARUDIO JIJINI MWANZA.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza, Miraji Mtaturu (Pichani), amewahikikishia wanachama wa Chama hicho kwamba CCM itaibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Marudio katika Kata za Isamilo Wilayani Nyamagana pamoja na Kitangiri Wilayani Ilemela, Jijini Mwanza.

Kauli ya Mtaturu imekuja baada ya jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoani Mwanza kutengua ushindi wa Madiwani wa Chadema katika Kata hizo na kuamuru uchaguzi urudiwe baada ya wagombea wa CCM kufungua kesi mahakamani kulalamikia ushindi wao.

Katika Kata hizo, Mahakama imesema marejeo ya Uchaguzi yatafanyika haraka iwezekanavyo baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza tarehe ya Uchaguzi.

Katika kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi katika Kata ya Nyamanoro yaliyompa ushindi diwani wa Chadema, Mahakama ilitengua matokeo hayo na hivyo kumtangaza diwani wa CCM kuwa diwani wa Kata hiyo.

Hata hivyo madiwani wa Kata hizo, wamesema kuwa watakata rufaa kupinga maamuzi ya kutengua ushindi wao yaliyotolewa na Mahakama.

No comments:

Powered by Blogger.