SERIKALI YAAHIDI KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI WA MAZAO YA NGOZI NCHINI.
Judith Ferdinand, Mwanza
Serikali imejipanga kusaidia wajasiriamali pamoja na vyuo vinavyotoa elimu ya ujasiriamali wa kutumia malighafi za ngozi za wanyama, ili kuendeleza sekta ya ngozi ili kutoa ajira kwa vijana.
Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ujasiriamali wa kutumia ngozi katika chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) tawi la Mwanza.
Prof. Mkenda alisema, ili kuzalisha bidhaa bora za ngozi, inatakiwa vijana kupatiwa mafunzo yatakayosaidia kuendana na soko la kimataifa.
Mmoja wa wajasiriamali waliohudhuria mafunzo hayo Thobias Machele, amesema katika sekta ya uzalishaji bidhaa kwa kutumia ngozi wanakabiliwa na ukosefu wa mashine ambao ungesaidia kuokoa muda na kutoa vitu vilivyo bora.
No comments: