LIVE STREAM ADS

Header Ads

UZINDUZI WA DARAJA LA KIGAMBONI, MAGUFULI AMTUMBUA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Wilson Kabwe (Pichani) amesimamishwa kazi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli hii leo.

Uamuzi huo umekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda kulalamikia baadhi ya mikataba iliyosainiwa na halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ikiwemo ya uendeshaji wa Kituo cha Mabasi cha Ubungo kwamba ina mazingira ya rushwa jambo ambali linaiingiza Serikali katika hasara kubwa.

Hayo yamejiri katika shughuli ya uzinduzi wa daraja la Kigamboni ambalo Dkt.Magufuli amesema ni vyema daraja hilo likapewa jina la Nyerere (Hayati Baba wa Taifa, Mwl.Julius Kambarage Nyerere).
Mwonekano wa daraja la Kigamboni.

No comments:

Powered by Blogger.