LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIVA KARUME VIVA.

Ikiwa leo ni Miaka 44 ya kumbukumbu ya kuuawa kwa Muasisi wa Mapinduzi na Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume alieuawa Aprili 7, 1972, bado mchango wake katika kupigania ukombozi unakumbukwa sana.

Binagi Blog inaamini kwamba mchango wake utaendelea kukumbukwa vizazi kwa vizazi, si tu kwa mapinduzi ya Zanzibar bali pia katika kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar baada ya makubaliano baina yake na muasisi wa Uhuru wa Tanganyika, Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere.

Hakuna jibu la moja kwa moja ikiwa kuuawa kwako kulikuwa kwa kulipiza kisasi, ila risasi nne zilizotolewa mwilini mwako, inatosha kusema kwamba uliuawa kikatili sana na kwa mchango wako katika ukombozi wa Wanzanzibari hukustahili kufa kwa risasi. Mola ailaze roho yako pahali pema peponi. Daima Utakumbukwa Milele. Viva Karume Viva, kwani bado unaishi katika mioyo yetu.

No comments:

Powered by Blogger.