MKURUGENZI USHETU AWATOSA WAANDISHI WA HABARI.
Na:Shaban Njia
Wakati joto la uteuzi wa wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na wakuu wa Wilaya nchini likizidi kupanda, Mkurugenzi Halmashauri ya Ushetu Isabela Chirumba amesema hataki kuwaona Waandishi wa habari katika shughuli zake kwa madai kwamba wamekuwa wakiandika masuala mabaya tu juu yake.
Mhe.Chirumba alitoa kauli hiyo juzi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Vitta Kawawa, wakati wa makabidhiano ya madawati 1,200 yaliyotolewa na serikali kupitia Tamisemi kwa ajili ya Halmashauri zote tatu zinazounda Wilaya ya Kahama, Mkoani Shinyanga.
No comments: